DUA - Linatokana na lugha ya Kigirikii ' deesis' maana yake ni kuomba jambo maalumu kwa kusihi
Kwa hiyo dua ni ombi maalumu kwa kumsihi Mungu. Tunaweza kuona katika maandiko jinsi Yesu Kristo anatufundisha kuomba kwa bidii bila kukata tamaa na hatimaye kupata majibu. Imeandikwa katika 'LUKA 18:7 - Na Mungu, je Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao'
'LUKA 18:8 - Nawaambia, atawapatia haki upesi walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je Ataiona imani duniani'
Pia tunaweza kujifunza kwa Bwana wetu Yesu Kristo wakati anakaribia mauti yake alifanya dua. Luka 22:42-44
42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.
43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
SALA—Linatokana na neno la Kigiriki ‘ProseuchÄ“ ‘Maana ya msingi: kuongea na Mungu kwa ibada au mawasiliano ya jumla.
Mathayo 6:9-139 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
MAOMBEZI - Maana yake ni kuomba kwa ajili ya wengine.
SHUKRANI - Linaltokana na neno la Kiebrania 'Yadah' maana yake kusema maneno ya shukrani. Tunaweza kuona ilivyoandikwa katika Waebrania 13:15 Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.
KUABUDU - Linatokana na neon la Kiebrania ' Shachah', Kwa hiyo, kibiblia yadah si tu kusema “asante,” bali linaweza na mara nyingine kwa tendo la kuinua mikono.
UPAKO - Ni kumiminiwa mafuta, kutengwa au kuwekwa wakfu kwa ajili ya kazi maalum ya Mungu, kama ya ukuhani, ufalme na nabii.
1 Wafalme 19:15-16,15
Bwana akamwambia, Enenda, urudi njia ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu.
16 Na Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako.
Kutoka 30:30 Nawe utawatia mafuta Haruni na wanawe, na kuwatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
Luka 4:18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Maoni
Chapisha Maoni