Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUKUMBUKWA NA MUNGU

Kuna watumishi wa Mungu katika biblia ambao walikumbukwa na Mungu. Ni kwa sababu walikuwa na sifa njema mbele zake. Mojawapo ya sifa hizo, walikuwa wameyatoa maisha yao kwake ili kumpendeza. Kwa sababu hiyo Waliisha sawasawa na neno lake. 

Walikuwa wakitii kwa kila neno ambalo Mungu aliwaagiza, ndio maana wamekumbukwa kwa  ajili ya mema yao katika vizazi vingi. Kwa sababu hiyo watu kama hao Mungu alipendezwa nao.

Wamekuwa kielelezo kwa watu wengine. Watu kama hao wakiondoka hapa duniani watakumbukwa. 

Hapa nitawataja baadhi ya watu katika biblia ambao wamekumbukwa  ni Ibraimu, Musa na Daudi.

Ni vema kufahamu ya kwamba mtu mwenye sifa njema, amepanda wema katika maisha yake na vizazi vyake. 

Kwa soma hili tunajifunza ya kwamba yatupasa tuangalie jinsi tunavyo enenda mbele za Mungu. Ili tukiondoka hapa duniani tuache sifa njema mbele za Mungu na wanadamu. Kwa sababu ya sifa njema uzao wako unabarikiwa.

Kuna watu wengine hawakutii maagizo yake wamekumbukwa kwa ajili ya makosa yao kwa vizazi vingi. Hao waliacha sifa mbaya. Hapa nitamtaja mmoja wapo ambaye ni Mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati. Alitajwa mara nyingi kwa maovu yake aliyoyatenda ambayo yameandikwa katika vitabu vya Wafalme wa kwanza  na Wafalme wa pili.

Jambo la kukumbuka.Ili Mungu akukumbuke yakupasa kuwa na sifa njema. Ambayo inatokana na kuyatii maagizo yake.

Shirikisha wengine somo hili.Mungu akubariki.

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...