Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NYIMBO ZA KUMTUKUZA MUNGU 2.

Jambo la kwanza na muhimu inampasa  mkristo kutambua ya kwamba Mungu alimuumba mwanadamu kwa kusudi maalum. Kwa hiyo, sababu mojawapo ni ili mwanadamu amtukuze kwa sifa na nyimbo. Kwa sababu hiyo Mungu anapenda sifa, ndio maana imeandikwa yeye huketi katika sifa. “Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.” Zaburi 22:3. “Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.” Zaburi 150:6.

Pia viumbe vyote na vitu vyote ambavyo Mungu aliviumba humsifu yeye. “Na kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.” Ufunuo wa Yohana 5:13.
“Haleluya.
Msifuni BWANA kutoka mbinguni; Msifuni katika mahali palipo juu. Msifuni, enyi malaika wake wote; Msifuni, majeshi yake yote.
Msifuni, jua na mwezi;
Msifuni, nyota zote zenye mwanga. Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu. Na vilisifu jina la BWANA, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.Amevithibitisha hata milele na milele, Ametoa amri wala haitapita. Msifuni BWANA nchi, Enyi nyangumi na vilindi vyote. Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba ulitendao neno lake. Milima na vilima vyote, Miti yenye matunda na mierezi yote. Hayawani, na wanyama wafugwao, Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa Wafalme wa dunia, na watu wote, Wakuu, na makadhi wote wa dunia Vijana waume, na wanawali,
Wazee, na watoto; Na walisifu jina la BWANA, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.” Zaburi 148:1-13.

Hapa nitazitaja aina ya sifa ni kama ifuatavyo:
1.Kuna sifa kwa ajili ya  Mungu. Ni zile sifa ambazo humwelekea Mungu moja kwa moja yeye pekee wakati watakatifu wapomsifu. Ili sifa zimwelekee ni pale mkristo anapomsifu Mungu kuhusu Ukuu wake, Mamlaka yake, Utakatifu wake, Rehema zake, Neema zake, fadhili zake, Upendo wake na kadhalika.

Pia kuna jambo lingine la msingi na kuzingatia yatupasa kumsifu na kumwimbia Mungu kwa kufuata kanuni ya neno lake. Kwa hiyo neno la Mungu ndiyo kielelezo au dira ya kutuongoza jinsi itupasavyo kumsifu Mungu sawasawa na neno lake.

Jinsi ya kumsifu na kumwimbia Mungu kwa usahihi. Mkristo anaweza kujifunza kupitia sifa na nyimbo zile ambazo zimeaandikwa katika Biblia.
“…..Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.” Ufunuo wa Yohana 5:12. 2. “...hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA,” Mambo ya Nyakati 5:13.
2. Kuna sifa ambazo siyo kwa ajili ya kumsifu Mungu. Ni zile sifa ambazo mtu hupewa na wanadamu. Tukiangalia katika Biblia kuna watumishi wa Mungu Daudi na Sauli ambao walisifiwa na wanawake kwa nyimbo. “Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.” 1Samweli 18:7.

3.Kuna sifa na  nyimbo ambazo si sahihi kuimba. Kwa sababu haziendani na neno la Mungu. Nyimbo ambazo hazifai kuimbwa nitazitaja na kuzitolea maelezo ili mtu aweze kuelewa. Kuna wimbo wa kumsifu Mungu ambao unasema; 

Hakuna Mungu kama wewe x3
 Hakuna na hata kuwepo
nimetembea (kote x2)
nimezunguka (kote x2)
nimetafuta (kote x2)
 Hakuna na hata kuwepo.

Huu wimbo ukiutafakari kwa makini utagundua hakuna ukweli ya kwamba mtu ametembea kote, amezunguka kote, na ametafuta kote. Kwa sababu hiyo huo ni uwongo. 


Nyimbo za tenzi.

Baadhi ya nyimbo za tenzi si sahihi. Kwa hiyo ni muhimu kwa kila mkristo ambaye ameokoka kuwa makini na kuhakikisha kuhusu sifa na nyimbo anazomwimbia  Mungu kuwa ni sahihi. Bofya hapa kufuatilia sehemu ya kwanza ya somo Hili

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...