Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NYIMBO ZA KUMTUKUZA MUNGU 1.

Jambo  la  kwanza  na  muhimu  ambalo  inatupasa  tulifahamu  ni  kwamba  Mungu  alituumba  ili tumtumikie  kwa  kulitii  neno  lake  linavyosema,  pamoja  na  kuimba  na  kusifu  mbele  zake.  Ili mtu  aweze  kulitii  neno  la  Mungu  ni  lazima  ajifunze  na  kuzijua  kanuni.  Pia  katika  kuimba  na kusifu  kuna  kanuni  zake.  Mtu  ambaye  amefanikiwa  katika  mambo  ya  Mungu  sana  ni  yule anayezingatia  kanuni  za  neno  la  Mungu.  Tukiangalia  katika  uumba  tunaona  wazi  ya  kwamba Mungu  aliviumba  vitu  vyote  katika  kanuni. Na  kila  mtu  aliyeokoka  yampasa  kujifunza  kwa  bidii  na  kuzijua  kanuni  zote  ambazo  ziko katika  neno  la  Mungu  na  kuzingatia.   Ili  mtu  aweze  kuimba  na  kusifu  na  hata  Mungu  atukuzwe  kuna  kanuni  zifuatazo; 

1. Ni  lazima  awe  ni  mtu  anayeishi  maisha  ya  utakatifu.

A. Asiyeipenda  miziki  ya  dunia. Asiwe  mtu  ambaye  baada  ya  kuokoka  bado  anaipenda  miziki  ya  dunia  hii  na  mapigo  yake. Hapaswi  mtu  ambaye  ameokoka  kuipenda  miziki  ya  dunia  hii  na  kuihamishia  kanisani  kwa kuimba  na  kucheza  kwa  kunengua  kama  ilivyo  kwa    wana  wa  dunia.  Kama  bado  unayo  hali ya  kuipenda  namna  ya  uimbaji  na  uchezaji  wa  dunia  hii  geuka  na    kutubu  nawe utasamehewa. Ni  muhimu  kufahamu  ya  kwamba  hatupaswi  kuiga  namna  nyingine  zozote  nje  ya  neno  la Mungu.  Yatupasa  kuzingatia  kanuni  za  neno  la  Mungu  ambazo  zinatuongoza  jinsi  ya  kuimba na  kusifu  mbele  za  Mungu  ipasavyo.  
B. Usifanye  vitendo  visivyo  na  maana. Jambo  la  muhimu  na  kuzingatia  ni  kufahamu  jinsi  ipasavyo  kuimba,  kusifu,  kucheza  na kufanya  vitendo  vinavyofaa  na  kumpendeza  Mungu.  Wakati  mtu  anacheza  mbele  za Mungu  yampasa  afanye  yanayofaa.   

C. Kuimba  na  kusifu  si  kwa  mashindano  na  kujionyesha. Mtu  aliyeokoka  hapaswi  kuingia  katika  kongamano  la  mashindano  ya  waimbaji  kama  watu wasiomjua  Mungu.  Hatujaitiwa  kujionyesha  na  kushindana  ili  aonekane  ni  mwimbaji  yupi ambaye  anaimba  vizuri  zaidi  kuliko  wengine.  Afanyaye  hivyo  anakuwa  ameenda  kinyume  na neno  la  Mungu  na  kufanya  dhambi.

D. Usiifanyie  Karama  ya  Mungu    biashara.  Karama  au  kipawa  kwa  neema  yake  Mungu ametoa  bure  na  kumpa  kila  mtu  kama  apendavyo  yeye. Kwa  sababu  hiyo  katika  kanisa  kuna  wakristo  waliojaliwa  kuimba  na  kusifu  kwa  namna  ya ajabu  sana.  Lakini,  hawapaswi  kuzitumia  Karama  walizopewa  bure  kwa  kusudi  la kujipatie  mapato.  Vilevile  kwa  kuwa  kuna  Karama  nyingi  na  kila  mtu  ambaye  Mungu amempa  Karama  asiifanyie  biashara.  Imeandikwa;
“Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;” Mathayo 10:8-9


Ili kuendelea na sehemu ya pili ya somo hili bofya hapa, NYIMBO ZA KUMTUKUZA MUNGU 2.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...