Mkristo ambaye ameokoka na kusimama imara katika imani ya neno la Mungu na Utakatifu, ndiye anayeweza kuwasiliana na Mungu. Kwa hiyo mtu akiwa anamwomba Mungu ni njia mojawapo ya kuwasiliana naye. Ili kujenga mawasiliano yako na Mungu yakupasa kumwomba kila siku. Na ndivyo Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa akimwomba Mungu kila siku wakati alipokuwa hapa duniani. Kwa hiyo yeye ni kielelezo katika maisha yetu kuhusu kuomba. Pia kuna njia zingine za kuwasiliana na Mungu ambazo ni kumwimbia nyimbo za kumsifu na kumwabudu. Kwa sababu hiyo tambua ya kwamba hizo ni njia ambazo Mungu ameziweka ili mwanadamu aweze kuwasiliana naye kwa imani. Kila mkristo anayemwendea Mungu katika njia hizo ambazo nimezitaja hapa juu ni lazima amwendee Mungu kwa imani. Kwa kufanya hivyo Mungu atapendezwa naye na kumsikiliza. “Waebrania 11:6
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”
Pia tunawezaje kuona kuna njia ambazo Mungu huwasiliana na watu wake ni kama zifuatazo;
1 Kwa njia ya sauti.
2 Kwa njia ya maono.
3 Kwa njia ya ndoto.
4 kwa njia zilezile ambazo nimezitaja hapo juu. Mkristo akiwa anawasiliana na Mungu kwa njia ya maombi, kusfu na kuabudu Mungu husema naye. Lakini ikiwa anamtafuta Mungu kwa bidii na kudumu katika Utakatifu ndipo Mungu kwa kusudi lake atawasiliana naye na kusema naye. Tunaweza kuona wale mitume wa Yesu walipokuwa wanawasiliana na Mungu kwa kufanya ibada ya maombi na kufunga, Mungu alisema nao. Matendo ya Mitume 13:2-3 “Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.”
Sawa ni vema nimefundisha somo hili, si kwamba mkristo anapowasiliana na Mungu asubiri ili aseme naye. La hasha bali Mungu kwa kusudi lake atasema kwa wakati wake.
Amen, ahsanteni sana
JibuFutaAsante Amen
JibuFuta