Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NJIA ZA KUWASILIANA NA MUNGU.

Mkristo ambaye ameokoka na kusimama imara katika imani ya neno la Mungu na Utakatifu, ndiye anayeweza kuwasiliana na Mungu. Kwa hiyo mtu akiwa anamwomba  Mungu ni njia mojawapo ya kuwasiliana naye. Ili kujenga mawasiliano yako na Mungu  yakupasa kumwomba kila siku. Na ndivyo Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa akimwomba Mungu kila siku wakati alipokuwa hapa duniani. Kwa hiyo yeye ni kielelezo katika maisha yetu kuhusu kuomba. Pia kuna njia zingine za kuwasiliana na Mungu ambazo ni kumwimbia nyimbo za kumsifu na kumwabudu. Kwa sababu hiyo tambua ya kwamba hizo ni njia ambazo Mungu ameziweka ili mwanadamu aweze kuwasiliana naye kwa imani. Kila mkristo anayemwendea Mungu katika njia hizo ambazo nimezitaja hapa juu ni lazima amwendee Mungu kwa imani. Kwa kufanya hivyo Mungu atapendezwa naye na kumsikiliza. “Waebrania 11:6
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”

Pia tunawezaje kuona kuna njia ambazo Mungu huwasiliana na watu wake ni kama zifuatazo;
1 Kwa njia ya sauti.
2 Kwa njia ya maono.
3 Kwa njia ya ndoto.

4 kwa njia zilezile ambazo nimezitaja hapo juu. Mkristo akiwa anawasiliana na Mungu kwa njia ya maombi, kusfu na kuabudu Mungu husema naye. Lakini ikiwa anamtafuta Mungu kwa bidii na kudumu katika Utakatifu ndipo  Mungu kwa kusudi lake atawasiliana naye na kusema naye. Tunaweza kuona wale mitume wa Yesu walipokuwa wanawasiliana na Mungu kwa kufanya ibada ya maombi na kufunga, Mungu alisema nao. Matendo ya Mitume 13:2-3 “Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.”

Sawa ni vema nimefundisha somo hili, si kwamba mkristo anapowasiliana na Mungu asubiri ili aseme naye. La hasha bali Mungu kwa kusudi lake atasema kwa wakati wake.

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...