Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUSHINDA MAJARIBU YOTE.

Kitu cha kwanza mkristo aliyeokoka anapaswa kukijua ni kwamba hapa duniani kuna majaribu ya namna nyingi. Kwa sababu hiyo yule mwovu hutujaribu katika hayo. Lengo lake ni kututoa katika kusudi la Mungu ili tutende dhambi. Mtu ambaye anamcha Mungu kwa bidii ni rahisi sana kushinda majaribu yote. Tunaweza kuona katika maandiko ya kwamba Yesu Kristo ambaye ni Bwana wetu na Ayubu  walijaribiwa na Shetani. Walimshinda kwa sababu walikuwa wakimcha Mungu.
Kwa hiyo ili mkristo aweze kumshinda Shetani yapo mambo muhimu ya kujifunza katika neno la Mungu. Mambo hayo ni kama ifuatavyo;

1. Kulifahamu neno la Mungu. Ikiwa Mtu analifahamu neno la Mungu ni  jambo la muhimu sana. Tunajifunza kwa Yesu alivyojaribiwa na ibilisi na kushinda ni kwa sababu alikuwa analifahamu neno la Mungu linavyosema. Kwa sababu hiyo aliweza kuzitambua hila za Shetani na kumpinga. "Ibilisi akamwambia, .... liambie jiwe hili liwe mkate. Yesu akamjibu, Imeandikwa mtu ya kwamba hataishi kwa mkate tu." Luka 4:3-4. Pia Shatani alimjaribu Ayubu akapoteza watoto, watumishi na mali zake zote. Kwa sababu alikuwa anamfahamu Mungu kwa ukamilifu hakutenda dhambi. Ndio maana imeandikwa "Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu." Ayubu 1:22. Kuna umuhimu wa mwamini aliyeokoka ili kuyafahamu maandiko ya neno la Mungu yampasa kujifunza kwa bidii na kuyahifadhi moyoni. Ndipo anaweza kuzitambua hila za Shetani na kumpinga. Kuna umuhimu wa mwamini aliyeokoka ili kuyafahamu maandiko ya neno la Mungu yampasa kujifunza kwa bidii na kuyahifadhi moyoni. Ndipo anaweza kuzitambua hila za Shetani na kumpinga.
“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.” Wakolosai 3:16.

2. Kudumu katika maombi. "Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; ...." Mathayo 26:41. Ikiwa mtu anamwomba Mungu  kila siku ni rahisi kuzitambua hila za Shetani na kumshinda.

3. Kujilinda na kuepuka dhambi.
Ni muhimu kila mkristo aliyeokoka kuwa makini na kuyatambua mazingira yenye ushawishi wa  mambo maovu na kuyaepuka. Kwa kufanya hivyo hataingia majaribuni.  "....aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi." 1Yohana 5:18.
"Palikuwa na mtu....alikuwa aliitwa Ayubu....ni mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na maovu." Ayubu 1:1.

Maoni

  1. Bila jina21:57

    Mungu akubariki kwa somo zuri

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...