Neno kumcha Bwana lina maana ya kumwogopa au kumhofu Mungu. Tuangalie ni nani anaweza kuwa na hofu ya Mungu? Jibu la swali hili ni kwamba mtu anayeweza kumhofu Mungu ni yule ambaye ameamua kumpenda Mungu. Uthibitisho wa mtu anayempenda Mungu ni yule ambaye hufanya haya yafuatayo; .
1.Anaishi neno la Mungu linavyosema.
2. Ana bidii kufanya ibada kwa Mungu. Pia kwa njia ya maombi, kumsifu na kumwabudu Mungu.
3.Anachukia dhambi na kuziepuka.
4.Furaha yake ni kumwabudu Mungu. Asipofanya ibada anahisi amepungukiwa ile nafasi ya kukaa mbele za Bwana. Mtu wa namna hiyo anakuwa amemwishia Bwana.
Ndio maana imeandikwa, Zaburi 34:9 "Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, ....” Watakatifu ni wale watu ambao wamejitolea maisha yao kwa Mungu na kumpenda kuliko mambo yoyote ya dunia hii.
Tunaweza kujifunze kwa Yesu Kristo ambaye ndiye kielelezo alikuwa anamcha Mungu. Ndio maana imeandikwa katika Isaya 11:2-3 "Na roho ya Bwana atakaa juu yake, .... roho ya maarifa na kumcha Bwana; .... na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana;...”
Imeandikwa katika Mithali 16:6 ".... kwa kumcha Bwana watu hujiepusha na maovu.” Kutokana na andiko hilo linamaanisha watu walio na hofu ya Mungu hawatendi dhambi kwa sababu wanamwogopa Mungu. Ndiyo maana neno la Mungu linafundisha katika Zaburi 4:4 "mwe na hofu wala msitende dhambi, ...." Andiko hilo linasisitiza kwa watu wote, kuwa na hofu ya Mungu na kukataza kutenda dhambi. Wanadamu wote wanapaswa kumhofu Mungu na kila mtu kuuchunguza moyo wake kwa yale anayoyatenda. Je, unayoyatenda yanampendeza Mungu ?
Ikiwa mtu ataishi katika dhambi anakuwa hana hofu ya Mungu. Kwa sababu hiyo Mungu atamwacha kwa sababu hakai na mwenye dhambi. Yeye ni mtakatifu hukaa na watakatifu. Isaya 57:15
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
asante kwa mafundisho
JibuFutaMungu akuzidishie roho Hekima, ili tuzidi kujifunzq kwako
JibuFuta