Neno la Mungu katika Biblia linatufudisha kuhusu upendo wa Mungu kwetu. Yeye Mungu ndiye mwanzo wa upendo kwa sababu alitupenda kwanza.
“...alitupenda sisi kwanza”. 1 Yohana 4:19.
“...alitupenda sisi kwanza”. 1 Yohana 4:19.
Jinsi mtu anavyoweza kuwa na upendo wa Mungu. Ni pale mtu anapokuwa amezingatia kudumu katika upendo wa Mungu kama ifuatavyo;
1.Kuishi sawasawa na maagizo yote ya neno la Mungu na kumpenda. “Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;” Kumbukumbu la Torati 10:12. “Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwaamuru, kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote”. Yoshua 22:5.
2. Jambo lingine la kuzingatia ni kwamba yampasa mtu kuyashika maagizo ya neno la Mungu kwa upendo. “Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo”. Waefeso 4:15. “Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo”. 2 Yohana 1:6.
3. Wale ambao wameokoka wanapaswa kupendana kama Kristo alivyowapenda. Yesu aliagiza kwa kusema; “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. Yohana 13:34-35.
Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. Yohana 13:34-35.
4.Kuepuka kuipenda dunia na mambo yake. Mtu ambaye ameokoka anapaswa kumpendeza Mungu katika mambo yote. Hapaswi Kuwa na tamaa mbaya na kujipatia mali na fedha kwa njia isiyo ya halali. Au kufanya biashara ambazo ni kinyume na neno la Mungu. Kwa sababu hiyo mtu akifanya mambo ambayo ni kinyume na neno la Mungu hatakuwa na upendo wa Mungu ukikaa ndani yake, bali anaipenda dunia na vitu vilivyomo. “Msiipende dunia,wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”. 1 Yohana 2:15-17.
Kujifunza zaidi bofya hapa
Ubarikiwe
JibuFutaMUNGU akubariki kwakazi unayoifanya ninaendelea kumpenda MUNGU na kuongezeka kiimani🙏🙏
JibuFuta