Namshukuru Mungu kwa ajili ya wakati huu ambao amenijalia kuutumia kuandika somo hili ambalo linahusu upendo wa kwanza kupoa. Ili uweze kufahamu nitaeleza kwa uhalisi ya kwamba mtu anapokuwa ameokoka anakuwa na hamasa ndani ya moyo wake, au kwa maneno mengine naweza kusema anakuwa na shauku, kiu na hamu kwa ajili ya mambo ya Mungu. Huo ndio upendo wa kwanza. Mtu wa namna hiyo inaonesha wazi anampenda Mungu. Kwa sababu hiyo anakuwa na bidii ya kujifunza neno la Mungu, na kuutafuta uso wa Mungu kwa maomba, kumwabudu na kumsifu kila wakati. Kuwa hiyo ikiwa Mkristo aliyeokoka anafanya hayo anakuwa amedumu katika ule upendo wa kwanza.
Kuacha upendo wa kwanza.
Mkristo ambaye ameokoka yampasa kuwa makini asije akaacha kuwa na upendo wa kwanza kwa ajili ya shughuli za dunia na udanganyifu wa yule mwovu. Hapa nitaonesha mambo ambayo ni sababu ya mtu kuacha upendo wa kwanza ambazo ni kama ifuatavyo;
1. Kufanya dhambi au kuishi katika dhambi.
2.Shughuli za dunia hii. Kutokana na shughuli za kila siku mtu anakuwa hana muda wa kumtafuta Mungu. Kwa hiyo Mtu anapotumia muda mwingi katika mambo yake bila kuutafuta uso wa Mungu anakuwa ameuacha upendo wa kwanza.
3.Kutumia mitandao bila kuwa na kiasi.
Kama mtu atakuwa anatumia mitandao ya intaneti bila kuwa na kiasi cha muda wa kikomo anaweza kutumia muda mwingi zaidi kuliko kuwa na muda wa kutosha kumtafuta Mungu. Kwa sababu hiyo ni muhimu kutumia mitandao ya kijamii kwa kiasi, ambayo ni Facebook, WhatsAp na Instagram. Hii ni baadhi ya mitandao michache nimeitaja hapa. Jambo lingine ambalo ni kinyume na Mungu haiwezekani ukaipenda mitandao na mambo mengine na kujishughulisha nayo kuliko Mungu. Katika maisha yetu jambo la muhimu ni kumpa Mungu nafasi ya kwanza. Na pia katika jambo lolote kabla ya kulifanya yakupasa kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yako. Kwa hiyo Kila siku asubuhi mtu anapoamka kabla ya kufanya shughuli yoyote ni jambo la muhimu kumpa Mungu nafasi ya kwanza kwa kufanya ibada. Mtumishi wa Mungu Paulo alikuwa anafahamu ya kwamba hilo ni jambo la muhimu kabla ya mambo yote. Ndio maana aliagiza na kusema; “Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu” Timotheo 2:1-2.
Kutokana na andiko hili hapa juu yakupasa kufanya dua, sala, maombezi na shukrani kama ifuatavyo;
A.Kuomba kwa ajili yako na kwa ajili ya familia yako.
B.Kuomba kwa ajili mambo yote ili Mungu akusaidie na kukuongoza. “Nafsi zetu zinamngoja BWANA; Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu”. Zaburi 33:20. “Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.” Isaya 58:11.
C.Kuomba kwa ajili ya wengine.
D.Kumshukuru Mungu kwa ajili ya mambo yote ambayo umeomba kwake. "Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu". 1 Wathesalonike 5:18.
Matokeo ya mtu kupoa na kutokuwa na upendo wa kwanza ni haya yafuatayo;
1. Mtu ambaye amepoa anapoteza uhusiano wake wa kuwa karibu na Mungu katika maisha yake. Pia anakuwa amepoteza hofu ya Mungu.
2. Anakuwa hajali mambo ya Mungu, bali anajali mambo yake zaidi kuliko ya Mungu. Mtu wa namna hiyo anakuwa ameyazoea mambo ya Mungu. Ndani ya moyo wake hana unyenyekevu wala kupondeka.
3. Anakuwa hana ile shauku au hamu ya kupenda mambo ya Mungu kama kuomba na kusoma neno la Mungu.

aliyemwamini Yesu na kuzaliwa mara ya pili ni muhimu kufahamu ya kwamba yampasa kuomba katika mapenzi ya Mungu. Ina maana kuomba kulingana na neno la Mungu. Hapa nitatoa mfano wa mtu anayeomba vibaya na kinyume neno la Mungu. Ni pale mtu ambaye ni mwizi anaomba Mungu amfanikishe kuiba fedha ya mtu mwingine.
Matokeo ya mtu kupoa na kutokuwa na upendo wa kwanza ni haya yafuatayo;
1. Mtu ambaye amepoa anapoteza uhusiano wake wa kuwa karibu na Mungu katika maisha yake. Pia anakuwa amepoteza hofu ya Mungu.
2. Anakuwa hajali mambo ya Mungu, bali anajali mambo yake zaidi kuliko ya Mungu. Mtu wa namna hiyo anakuwa ameyazoea mambo ya Mungu. Ndani ya moyo wake hana unyenyekevu wala kupondeka.
3. Anakuwa hana ile shauku au hamu ya kupenda mambo ya Mungu kama kuomba na kusoma neno la Mungu.
Kujifunza zaidi bofya hapa; dua, sala na maombezi.
Maoni
Chapisha Maoni