Jambo la kwanza na muhimu ambalo inatupasa tulifahamu ni kwamba Mungu alituumba ili tumtumikie kwa kulitii neno lake linavyosema, pamoja na kuimba na kusifu mbele zake. Ili mtu aweze kulitii neno la Mungu ni lazima ajifunze na kuzijua kanuni. Pia katika kuimba na kusifu kuna kanuni zake. Mtu ambaye amefanikiwa katika mambo ya Mungu sana ni yule anayezingatia kanuni za neno la Mungu. Tukiangalia katika uumba tunaona wazi ya kwamba Mungu aliviumba vitu vyote katika kanuni. Na kila mtu aliyeokoka yampasa kujifunza kwa bidii na kuzijua kanuni zote ambazo ziko katika neno la Mungu na kuzingatia. Ili mtu aweze kuimba na kusifu na hata Mungu atukuzwe kuna kanuni zifuatazo;
1. Ni lazima awe ni mtu anayeishi maisha ya utakatifu.
A. Asiyeipenda miziki ya dunia. Asiwe mtu ambaye baada ya kuokoka bado anaipenda miziki ya dunia hii na mapigo yake. Hapaswi mtu ambaye ameokoka kuipenda miziki ya dunia hii na kuihamishia kanisani kwa kuimba na kucheza kwa kunengua kama ilivyo kwa wana wa dunia. Kama bado unayo hali ya kuipenda namna ya uimbaji na uchezaji wa dunia hii geuka na kutubu nawe utasamehewa. Ni muhimu kufahamu ya kwamba hatupaswi kuiga namna nyingine zozote nje ya neno la Mungu. Yatupasa kuzingatia kanuni za neno la Mungu ambazo zinatuongoza jinsi ya kuimba na kusifu mbele za Mungu ipasavyo.
B. Usifanye vitendo visivyo na maana. Jambo la muhimu na kuzingatia ni kufahamu jinsi ipasavyo kuimba, kusifu, kucheza na kufanya vitendo vinavyofaa na kumpendeza Mungu. Wakati mtu anacheza mbele za Mungu yampasa afanye yanayofaa.
B. Usifanye vitendo visivyo na maana. Jambo la muhimu na kuzingatia ni kufahamu jinsi ipasavyo kuimba, kusifu, kucheza na kufanya vitendo vinavyofaa na kumpendeza Mungu. Wakati mtu anacheza mbele za Mungu yampasa afanye yanayofaa.
C. Kuimba na kusifu si kwa mashindano na kujionyesha. Mtu aliyeokoka hapaswi kuingia katika kongamano la mashindano ya waimbaji kama watu wasiomjua Mungu. Hatujaitiwa kujionyesha na kushindana ili aonekane ni mwimbaji yupi ambaye anaimba vizuri zaidi kuliko wengine. Afanyaye hivyo anakuwa ameenda kinyume na neno la Mungu na kufanya dhambi.
Ili kuendelea na sehemu ya pili ya somo hili bofya hapa, NYIMBO ZA KUMTUKUZA MUNGU 2.
Maoni
Chapisha Maoni