- KUSUDI LA KUHUBIRI INJILI
- kuna mambo ambayo mwalimu wa neno la mungu lazima kuyajua na kuzingatia wakati anapowafundisha waamini neno la mungu. mambo hayo ni haya maneno;
1.Kurudia kuyataja maandiko.
Mwalimu waamini maandiko ya kusoma katika biblia ni muhimu aweze kurudia rudia na kusubiri kidogo ili waamini waweze kufungua Biblia. Kwa kuzingatia kanuni hii inawapa nafasi wale ambao hawajasikia au sii wepesi kufungua maandiko kwa har aka. kwa hiyo kwa kufanya hivyo inakuwa rahisi kila kujifunza na kuelewa.
Kama mwalimu hata kuzingatia kanuni hizo baadhi ya waamini watashindwa kujifunza na kuelewa
2. Kumia maneno rahisi.
Mwalimu akifundisha kwa kutumia
maneno ambayo ni rahisi kwa kila mwamini aweze kuelewa neno la Mungu.
3. Kufundisha kwa ufupi.
Ni muhimu kutumia vipengele vifupi au maneno mafupi.
Kufundisha kwa namna hii inakuwa ni rahisi kuelewa na kulishika neno la Mungu.
4. kutumia mifano.
Kufundisha kwa kutumia mifano rahisi. Kwa hiyo kwa kupitia huduma mwamini kuelewa kwa urahisi. Ndio maana Yesu alikuwa anatumia mifano alipokuwa anafundisha.
Mtumishi wa Mungu ambaye ana karama ya kufundisha neno la Mungu na kuzingatia kanuni hizi atasababisha waamini kusikiliza anasababisha waamini kusikiliza kwana kuelewa.
Watumishi wa namna hii wanapata kibali katika kanisa kwa sababu wanafundisha kwa namna rahisi.
Amen barikiwa sana
JibuFutaNime Barikiwa na hii mbinu
JibuFuta