Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MWALIMU WA NENO LA MUNGU.

  • KUSUDI LA KUHUBIRI INJILI
  • kuna mambo ambayo mwalimu wa neno la mungu lazima kuyajua na kuzingatia wakati anapowafundisha waamini neno la mungu. mambo hayo ni haya maneno;
1.Kurudia kuyataja maandiko.
Mwalimu waamini maandiko ya kusoma katika biblia ni muhimu aweze kurudia rudia na kusubiri kidogo ili waamini waweze kufungua Biblia. Kwa kuzingatia kanuni hii inawapa nafasi wale ambao hawajasikia au sii wepesi kufungua maandiko kwa har aka. kwa hiyo kwa kufanya hivyo  inakuwa rahisi kila kujifunza na kuelewa.

Kama mwalimu hata kuzingatia kanuni hizo baadhi ya waamini watashindwa kujifunza na kuelewa 

2. Kumia maneno rahisi.
Mwalimu akifundisha kwa kutumia
maneno ambayo ni rahisi kwa kila mwamini aweze kuelewa neno la Mungu.

3. Kufundisha kwa ufupi.
Ni muhimu kutumia vipengele vifupi au maneno mafupi. 
Kufundisha kwa namna hii inakuwa ni rahisi kuelewa na kulishika neno la Mungu.

4. kutumia mifano.
Kufundisha kwa kutumia mifano rahisi. Kwa hiyo kwa kupitia huduma mwamini kuelewa kwa urahisi. Ndio maana Yesu alikuwa anatumia mifano alipokuwa anafundisha.  

Mtumishi wa Mungu ambaye ana karama ya kufundisha neno la Mungu na kuzingatia kanuni hizi    atasababisha waamini kusikiliza anasababisha waamini kusikiliza kwana kuelewa. 

Watumishi wa namna hii wanapata kibali katika kanisa kwa sababu wanafundisha kwa namna rahisi.

Maoni

  1. Bila jina23:46

    Amen barikiwa sana

    JibuFuta
  2. Bila jina20:35

    Nime Barikiwa na hii mbinu

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...