Fuatana
nami katika somo hili ambalo ni la muhimu sana katika maisha yako ya hapa
duniani na mbinguni. Mungu anatafuta mtu aliye mwaminifu ili amtumie
katika kazi yake. Na pia ili mtu aingie mbinguni yampasa kuwa mwaminifu. Ikiwa
mtu ni mwaminifu naye huaminiwa na Mungu na wanadamu. Hebu tuangalie ni nani
aliye mwaminifu? Jibu la swali hili ni mtu yule awekaye nia moyoni mwake na
kuzingatia kuyafanya yote aliyoagiza Mungu katika neno lake. Mtu huyu
anakubalika mbele za Mungu na wanadamu. Anakubalika kwa sababu
anampendeza Mungu na wanadamu katika kutenda yaliyo haki. Na ndio maana imeandikwa; "Mwanamgu, usisahau sheria yangu, Bali moyo wako
uzishike amri zangu. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu
na mbele za wanadamu". Mithali 3:1,4. "Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo,
akimpendeza Mungu na wanadamu." Luka
2:52.
Tunaweza kujifunza uaminifu kwa mtumishi wa Mungu Ayubu ambaye aliepuka dhambi na wala hakutenda dhambi. Naye Mungu alimwona ni mkamilifiu na kumhesabia kuwa ni mwenye haki. Na ndio maana Mungu alimuuliza swali shetani na kumthibitishia ya kwamba Ayubu ni mtu mkamilifu "Kisha Bwana akamuuliza Shetani, Je! umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na uelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu." Ayubu 1:8. Ili mtu aweze kudumu katika uamimifu kwanza inampasa kuchukia dhambi na kupenda kutenda yaliyo ya haki. Na pia inampasa kuweka nia moyoni ya kwamba ameamua kujilinda na kuepuka kutenda dhambi;
"...bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi."Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu (aliyeokoka) hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi." Yohana 5:18.
Kwa sababu Ayubu alikuwa ni mtu mwaminifu Mungu alimbarikia kuwa na mali nyigi, watoto na wafanyakazi wengi sana. Alimlinda Ayubu na watu wote aliokuwa nao nyumbani mwake. Pia alilinda kila kitu alichokuwa nacho. Ndio maana shetani asingeweza kumduru, ndipo Shetani akamwambia Mungu, "Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi." Ayubu 1:10. Mungu alimwinua Ayubu akumfanya kuwa mtu mkuu mwenye mali nyingi kuliko watu wote wa nchi ya Usi upande wa mashariki. Soma zaidi katika Biblia, Ayubu 1:2-3.
Tunaendelea kujifunza kuhusu uaminifu wa Ayubu. Alipojaribiwa na shetani watoto wake wakafa, mali zake zikaibwa na katika mwili wake akatokewa majipu. Hata hivyo aliendelea kudumu katika uaminifu wala hakutenda dhambi. Ila alivumilia na kumtumaini Mungu kama ilivyoandkwa, "Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, ambao hautatikisika, wakaa milele." Zaburi 135:1. "...Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu...hakufanya dhambi kwa midomo yake." Ayubu 1:13-22; Ayu 2:9-10.
Baada ya kujaribiwa Mungu alimponya na kumbarikia zaidi ya hayo aliyokuwa nayo mwanzo. "...Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo mwanzo..." Ayubu 42:10,12.
Vilevile Yesu na Musa walikuwa waaminifu katika mambo yote ya Mungu. "...Yesu aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa katika nyumba yote ya Mungu. Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye."
Waebrania 3:1-2, 5.
Yusufu naye alikuwa mtu mwaminifu aliyepuka dhambi. Kutokana na uaminifu wa Yusufu Mungu alimbarikia katika kazi alizokuwa akifanya katika nyumba ya mwajiri wake Potifa. Ndipo Potifa akafahamu ya kwamba Bwana yu pamoja na Yusufu na ndio maana nyunba yake imebarikiwa. Akamweka awe msimamizi mkuu wa myumba na vyote alivyo navyo. Na baadaye Mungu alimwinua na kumjalia kuwa mtu mkuu katika utawala wa Farao. Soma katika Biblia, Mwanzo 39:1-12; 41: 41,44.
Neno hio imekuwuwa ya baraka sana kwangu
JibuFutaTumebarikiwq
JibuFutaNeno limekuwa baraka kwangu
JibuFuta