Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MUNGU HUWATUMIA NA KUWABARIKI WALIO WAAMINIFU.

Fuatana nami katika somo hili ambalo ni la muhimu sana katika maisha yako ya hapa duniani na mbinguni. Mungu anatafuta mtu aliye mwaminifu ili amtumie katika kazi yake. Na pia ili mtu aingie mbinguni yampasa kuwa mwaminifu. Ikiwa mtu ni mwaminifu naye huaminiwa na Mungu na wanadamu. Hebu tuangalie ni nani aliye mwaminifu? Jibu la swali hili ni mtu yule awekaye nia moyoni mwake na kuzingatia kuyafanya yote aliyoagiza Mungu katika neno lake. Mtu huyu  anakubalika mbele za Mungu na wanadamu. Anakubalika kwa sababu anampendeza Mungu na wanadamu katika kutenda yaliyo haki. Na ndio maana imeandikwa; "Mwanamgu, usisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele za wanadamu". Mithali 3:1,4. "Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu." Luka 2:52.

Tunaweza kujifunza uaminifu kwa mtumishi wa Mungu Ayubu ambaye aliepuka dhambi na wala hakutenda dhambi. Naye Mungu alimwona ni mkamilifiu na kumhesabia kuwa ni mwenye haki. Na ndio maana Mungu alimuuliza swali shetani na kumthibitishia  ya kwamba Ayubu ni mtu mkamilifu "Kisha Bwana akamuuliza Shetani, Je! umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na uelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu." Ayubu 1:8. Ili mtu aweze kudumu katika uamimifu kwanza inampasa kuchukia dhambi na kupenda kutenda yaliyo ya haki. Na pia inampasa kuweka nia moyoni ya kwamba ameamua kujilinda na kuepuka kutenda dhambi; 

"...bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi."Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu (aliyeokoka) hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi." Yohana 5:18.

Kwa sababu Ayubu alikuwa ni mtu mwaminifu Mungu alimbarikia kuwa na mali nyigi, watoto na wafanyakazi wengi sana. Alimlinda Ayubu na watu wote aliokuwa nao nyumbani mwake. Pia alilinda kila kitu alichokuwa nacho. Ndio maana shetani asingeweza kumduru, ndipo Shetani akamwambia Mungu, "Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi." Ayubu 1:10.  Mungu alimwinua Ayubu akumfanya kuwa mtu mkuu mwenye mali nyingi kuliko watu wote wa nchi ya Usi upande wa mashariki. Soma zaidi katika Biblia, Ayubu 1:2-3.

Tunaendelea kujifunza kuhusu uaminifu wa Ayubu. Alipojaribiwa na shetani watoto wake wakafa, mali zake zikaibwa na katika mwili wake akatokewa majipu. Hata hivyo aliendelea kudumu katika uaminifu wala hakutenda dhambi. Ila alivumilia na kumtumaini Mungu kama ilivyoandkwa, "Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, ambao hautatikisika, wakaa milele." Zaburi 135:1. "...Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu...hakufanya dhambi kwa midomo yake." Ayubu 1:13-22; Ayu 2:9-10.

Baada ya kujaribiwa Mungu alimponya na kumbarikia zaidi ya hayo aliyokuwa nayo mwanzo. "...Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo mwanzo..." Ayubu 42:10,12.

 Vilevile Yesu na Musa walikuwa waaminifu katika mambo yote ya Mungu. "...Yesu aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa katika nyumba yote ya Mungu. Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye."

  Waebrania 3:1-2, 5.

Yusufu naye alikuwa mtu mwaminifu aliyepuka dhambi. Kutokana na uaminifu wa Yusufu Mungu alimbarikia katika kazi alizokuwa akifanya katika nyumba ya mwajiri wake Potifa. Ndipo Potifa akafahamu ya kwamba Bwana yu pamoja na Yusufu na ndio maana nyunba yake imebarikiwa. Akamweka awe msimamizi  mkuu wa myumba na vyote alivyo navyo. Na baadaye Mungu alimwinua na kumjalia kuwa mtu  mkuu katika utawala wa Farao. Soma katika Biblia, Mwanzo 39:1-12;  41: 41,44.

Maoni

  1. Bila jina07:55

    Neno hio imekuwuwa ya baraka sana kwangu

    JibuFuta
  2. Bila jina16:06

    Tumebarikiwq

    JibuFuta
  3. Bila jina00:13

    Neno limekuwa baraka kwangu

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...