Ruka hadi kwenye maudhui makuu

HAKUNA LAANA NA MAPEPO KWA ALIYEOKOKA.

Karibu katika somo hili na kulifuatilia kwa makini nawe utajengwa na kuzidi kuimarika katika neno la Mungu. Nianze kwa kusema kuwa neno la Mungu ni njia, na ni nuru katika maisha yetu. Neno la Mungu limefananishwa na njia kwa sababu mtu akiishi sawasawa na neno  linavyosema anajua anakokwenda na kwamba anafuata njia sahihi na wala hatapotea kamwe. "Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru" (Yn 8:32). Sehemu nyingine neno limefananishwa na nuru. Ikiwa mtu anaishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema, mtu huyo  anatembea katika nuru kungali mchana wala  hatapotea njia. Kwa sababu hiyo neno la Mungu ndilo linatufundisha na kufahamu mambo yote ambayo Mungu alitukirimia katika Kristo Yesu. Mojawapo ya mambo hayo ni;

1. Alituweka huru kutoka laana zote za ukoo, familia na mababu wa zamani. Na si hivyo tu alituweka huru mbali na mikosi na balaa. Ni kwa sababu hiyo Yesu Kristo alifanyika laana itokanayo na torati  kwa ajili yetu. Ndiyo maana andiko linasema, "Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanyika laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa , Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti." (Gal 3:13). Kwa sababu hiyo hakuna laana kwa mtu ambaye ameokoka kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu na kutusamehe dhambi. "...Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli." (Yn 8:34, 36). Maandiko haya mawili hapa juu yanafundisha kuhusu kazi moja ya kuwekwa huru na kutengwa mbali na laana na dhambi. Na si hivyo tu, ila kwa upendo wa Mungu ulio mkuu kwetu alitutoa katika utawala wa nguvu za giza na kutuingiza katika ufalme wa Yesu. Kwa hiyo sasa, kwa  watu wote  waliomkubali na  kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao wanaishi katika ufalme wa Mungu pamoja na Yesu Kristo ambaye ni Mwana wake. "Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake" (Kol 1:13).

2. Kwa mtu ambaye amekwishaokoka mapepo hayana nafasi katika maisha yake. Kwa sababu amezaliwa kwa mara ya pili kwa roho na maji na pia amemwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake na kufanyika mwana wa Mungu. Vile vile akiishi sawasawa na neno lisemavyo, hakika hakuna pepo atakayemkaribia wala kuingia ndani yake. Yeye yuko huru mbali na pepo kwa sababu amekwisha kuokolewa kutoka mamlaka ya giza. Mtu ambaye ameokoka anakuwa ni kiumbe kipya kwa sababu ameyaaacha mambo ya zamani yasiyofaa (yaani dhambi). Huyo amezaliwa kwa roho na kufanyika upya roho yake, na kuwa na namna ya Mungu ya Utakatifu. "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! yamekuwa mapya" (2Kor 5:17)

Mtu ambaye anaweza kupagawa na pepo  ni yule anayeishi maisha ya dhambi. Atendaye dhambi anakuwa ametengana na Mungu na ndipo pepo wabaya humwingia na kuishi ndani yake. Ndiyo maana Yesu alionya na kusema madhara yatakayosabishwa na pepo baada ya kuondolewa ndani ya mtu. Lakini  ikiwa mtu hakuishi maisha ya utakatifu  pepo watamwingia tena na kufanya makao ndani yake. "Pepo amtokapo mtu...Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya"  (Mat 12:43-45.)

Maoni

  1. Bila jina23:32

    Amina sana Mtumishi wa Mungu akubariki katika kuifanya kazi yake,naomba somo la matumizi ya damu ya yesu na ulinzi juu ya

    watakatifu.

    JibuFuta
  2. Bila jina12:55

    Asante Sana kwa injili sahihi.Mungu aitwaye Jehovah akubariki katika Jina la Yesu Kristo Amen and amen.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...