Wema wa Mungu kwa wanadamu.
1.Hili ni tunda ambalo linaonyesha
wema wa Mungu kwa waovu na wenye haki, kwa sababu huwatendea mema. Wakristo ambao wameokoka
yawapasa kufanana na yeye kwa kuwatendea watu wote mema. “Ili mpate
kuwa kama wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake
waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.” Mt 5:45.
2.Vile vile ameonyesha wema wake kwa
kutuokoa. “Lakini wema
wake Mwokozi wetu Mungu, na
upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa.” Tit 3:4.
3.Anawavuta
kwa wema wake ili wenye dhambi watubu. “Au waudharau
wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue wema wa Mungu
wakuvuta upate kutubu?” Rum 2:4.
Yatupasayo
kuwatendea adui zetu.
1.Kuwasamehe na kuwaombea Baraka. “Wabarikini
wanaowaudi; barikini, wala msilaani.” Rum 12:14. “Lakini mimi nawaambia,
wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.” Mt 5:44. “Watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu;
bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi Baraka.” 1Pet 3:9.
2.Kuwatendea mema. “Msimlipe mtu
ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Lakini, adui yako
akiwa na njaa , mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia
makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa
wema.” Rum
12:17,20-21.
Kwa kufanya
hivyo Bwana anakuwa upande wetu akitusaidia na kuwalipa kisasi adui zetu. “Usiseme, Mimi
nitalipa mabaya; Mgojee Bwana, naye atakuokoa.” Mit 20:22. “ Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni
ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa,
anena Bwana.” Rum 12: 19. Bwana hatakawia kulipa kisasi
kwa sababu amesema, “Kisasi ni
change mimi, na kulipa; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo
yatakayowapata yatafanya haraka.” Kum 32:35.
Sharti
linalohusu kutenda wema
Mtu anapotenda wema si vema
kujionyesha au kutangaza ili watu wafahamu. “Angalieni
msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya
kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye wa mbinguni.” Mt 6:1. Kutokana na andiko hili
tunajifunza ya kwamba mema tuyatendayo ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Yeye
pekee ndiye anayestahi kutukuzwa kwa yale mema tuyatendayo. Ndio maana Mungu
ameonya akisema, “Mimi ni
Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine....” Isa 42:8.
Malipo kwa
watu watendao wema.
Wataurithi ufalme wa Mungu. “Hapo
atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote
pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote
watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo
na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume na mbuzi mkono wake wa kushoto.
Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, njooni, mliobarikiwa
na Bwana, urithini ufalme uliowekwa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana
nalikuwa na njaa, mkanipa chukula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa
mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja
kunitazama; nalikuwa kifungoni mkanijia.
Ndipo wenye
haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, nilini tulipokuona una njaa, tukakulisha,
au una kiu, tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha,
au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulikuona u mgonjwa, au kifungoni,
tukakujia? Na Mfalme akajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, mlivyowatendea
mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo,
mlinitendea mimi.” Mt 25:31-40.
Malipo kwa
watu wasiotenda wema.
Watahukumiwa na kuadhibiwa katika
mateso ya moto wa milele. “ Kisha
atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa,
mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayaria Ibilisi na malaka zake; kwa
maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na
kifungoni, msije kunitazama;
Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au kiu, au u mgeni, au u uchi au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadri msivyowatendea mmojawapo wa hao walio wadogo hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.” Mt 25:41-46.
Amina Barikiwa sana
JibuFuta