1. Yesu amepewa mamlaka ya
kuumba.
Yesu Kristo ni mtu wa pekee kwa
sababu Mungu amempa ukuu na mamlaka yote duniani na mbinguni kuliko manabii,
makuhani, wafalme na wote waliomtangulia na waliokuja baada yake, wala hakuna
mwingine yeyote aliyepewa mamlaka yote.Yeye ni juu ya yote alikuwako tangu
mwanzo kabla ya misingi ya ulimwengu na kuumbwa chochote.Yeye aliumba vyote
akiwa na Baba yake mbinguni.”Yesu akawaambia, Ami, amin, nawaambia, yeye
Ibrahimu asijakuwako mimi niko.” Yohana
8:58. “Hapo mwanzo kulikuwako na
neno,naye neno alikuwako kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu (Yesu), Huyo mwanzo alikuwako kwa
Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika” Yohana 1:1-3.
“Yesu akaja kwao akasema nao,
akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” Mathayo 28:18. “Kwa hiyo Mungu
alimwadhimisha mno, akamkirimia lile jina lipitalo kila jina; ili kwa jina la
Yesu kila goti lipigwe,la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya
nchi;na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu
Baba” Wafilipi
2:9-11.
2. Malaka ya kufufua na
kuhukumu.
“Tena Baba
hamhukumu mtu ye yote, amempa Mwana hukumu yote, ili watu wote wamheshimu Mwana
kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hakumheshimu Baba
aliyempeleka. Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.
Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo
makaburini watasikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo
wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”. Yohana 5:22,23;
27,28. “Yesu
akamwambia, mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa
atakuwa anaishi ” Yohana
11:25.
3.Mamlaka
juu ya vitu vyote pia amewekwa juu ya Ufalme na Enzi.
Mungu amemfanya awe na mamlaka
juu ya vitu vyote kwa mapenzi yake na kwa utukufu wake. “aliotenda katika Kristo alipomfufua
katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana
kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina
litajwalo,wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu
vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya
kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anaye kamilika kwa vyote
katika vyote” Waefeso
1:20-23.
4. Amepewa mamlaka kuwa kuhani mkuu
milele.
“Basi, iwapo
tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu Mwana wa Mungu na tuyashike
sana maungamo yetu.Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufaywa
kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe Mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. Kama
asemapo mahali pengine, Ndiwe kuhani milele kwa mfano wa Melkizedeki” Waebrania 4:14; 5:5, 6.
5. Amepewa mamlaka kufanya
miujiza na kuponya magonjwa.
“Yeye ni mponyaji wa magonjwa na
kila aina ya udaifu.Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu,
mabubu, vilema na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya, hata ule
mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima,
viwete wanakwenda, na vipofu wanaona wakamtukuza Mungu wa Israel” Mathayo 15:30, 31. Wewe
kama ni mgojwa au una udaifu wowote kitu cha msingi ni kumwamini yesu ni
mponyaji na utaona muujiza wa kuponywa kwako. Mwamini Mungu na Yesu kristo na
umwombe Mungu kupitia jina la Yesu atakuponya pia utaona Mungu ni wa ajabu.
Lakini kabla ya kumwomba Mungu ili akusikie ni lazima uweke nia ya kuungama au
kutubu dhambi zote na kuzicha wala usitende dhambi tena.Usije ukapatwa na baya
zaidi.
6. Amepewa mamlaka kuokoa na
kusamehe dhambi.
Amepewa mamlaka ya kuokoa watu
kutoka dhambini. Hapa inamaanisha mtu hawezi kujiokoa mwenyewe na kuwa safi na
salama mbele za Mungu ndio maana alimtuma Yesu aje duniani ili watu wote wa
kila taifa na kila kabila
waokolewe katika yeye. Ndio maana maandiko utakayoyasoma hapa chini
yanamaanisha wingi “Naye
atazaa Mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa
watu wake na dhambi zao. Mathayo1:21.“Wala
hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna jina jigine chini ya
mbingu walilopewa wanadhamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” Matendo 4:12. "Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa
Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, ... Mathayo 9:6.
ameni mbarikiwe
JibuFuta