Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAMLAKA.

1. Yesu amepewa mamlaka ya kuumba.
Yesu Kristo ni mtu wa pekee kwa sababu Mungu amempa ukuu na mamlaka yote duniani na mbinguni kuliko manabii, makuhani, wafalme na wote waliomtangulia na waliokuja baada yake, wala hakuna mwingine yeyote aliyepewa mamlaka yote.Yeye ni juu ya yote alikuwako tangu mwanzo kabla ya misingi ya ulimwengu na kuumbwa chochote.Yeye aliumba vyote akiwa na Baba yake mbinguni.”Yesu akawaambia, Ami, amin, nawaambia, yeye Ibrahimu asijakuwako mimi niko.” Yohana 8:58. “Hapo mwanzo kulikuwako na neno,naye neno alikuwako kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu (Yesu), Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika” Yohana 1:1-3.  
                                             
“Yesu akaja kwao akasema nao, akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” Mathayo 28:18. “Kwa hiyo Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia lile jina lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe,la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba” Wafilipi 2:9-11. 

2. Malaka ya kufufua na kuhukumu.
Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, amempa Mwana hukumu yote, ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hakumheshimu Baba aliyempeleka. Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini watasikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”. Yohana  5:22,23; 27,28. “Yesu akamwambia, mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa atakuwa anaishi ” Yohana 11:25.  

3.Mamlaka juu ya vitu vyote pia amewekwa juu ya Ufalme na Enzi. 
Mungu amemfanya awe na mamlaka juu ya vitu vyote kwa mapenzi yake na kwa utukufu wake. “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo,wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anaye kamilika  kwa vyote katika vyote” Waefeso 1:20-23.

4. Amepewa mamlaka kuwa kuhani mkuu milele.
Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu Mwana wa Mungu na tuyashike sana maungamo yetu.Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufaywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe Mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. Kama asemapo mahali pengine, Ndiwe kuhani milele kwa mfano wa Melkizedeki” Waebrania 4:14; 5:5, 6.

 5. Amepewa mamlaka kufanya miujiza na kuponya magonjwa.
“Yeye ni mponyaji wa magonjwa na kila aina ya udaifu.Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya, hata ule mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona wakamtukuza Mungu wa Israel” Mathayo 15:30, 31. Wewe kama ni mgojwa au una udaifu wowote kitu cha msingi ni kumwamini yesu ni mponyaji na utaona muujiza wa kuponywa kwako. Mwamini Mungu na Yesu kristo na umwombe Mungu kupitia jina la Yesu atakuponya pia utaona Mungu ni wa ajabu. Lakini kabla ya kumwomba Mungu ili akusikie ni lazima uweke nia ya kuungama au kutubu dhambi zote na kuzicha wala usitende dhambi tena.Usije ukapatwa na baya zaidi.

6. Amepewa mamlaka kuokoa na kusamehe dhambi.
Amepewa mamlaka ya kuokoa watu kutoka dhambini. Hapa inamaanisha mtu hawezi kujiokoa mwenyewe na kuwa safi na salama mbele za Mungu ndio maana alimtuma Yesu aje duniani ili watu wote wa kila taifa na kila kabila waokolewe katika yeye. Ndio maana maandiko utakayoyasoma hapa chini yanamaanisha wingi  “Naye atazaa Mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Mathayo1:21.“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna jina jigine chini ya mbingu walilopewa wanadhamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” Matendo 4:12. "Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, ... Mathayo 9:6.

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...