Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAANA YA MANENO KATIKA BIBLIA.

D UA-  Linatokana na neno la Kiyunani ' deesis'  maana yake kuomba kwa bidii na kwa nguvu zote mpaka majibu yanapokuwa yamepatikana. Maana ya dua ni mabadiliko hoja nzito mbele za Mungu na kuendelea kuhojiana na Mungu mpaka upate majibu yako. Tunaweza kuona katika maandiko jinsi Yesu Kristo anatufundisha kuomba kwa bidii bila kukata tamaa na kuu haki upesi. Neno kubwa haki upesi linamaanisha joto upesi ulicho kiomba au uliyo yaomba. Maandiko yanayohusiana na hayo unaweza kuona kwenye sanduku la Biblia,  Luka 11: 5-10; 18: 1-8; Yakobo 5: 17-18; Wakolosai 1: 9.

Yeye mwenyewe Bwana wetu Yesu Kristo wakati anakaribia mauti yake ya kwanza maombi na dua pamoja na kulia sana kwa machozi akasikilizwa kwa kuwa alikuwa Mungu wa Mungu na kujifunza kuwa. Mara Malaika akamtia nguvu, Soma katika Biblia,  Waebrania 5: 7-8; Luka 22: 39-44.  Sisi vile vile inatupasa kumcha Mungu yaani kumhofu na wewe neno ziwa na kwamba wewe kwa kufanya linavyosema ndipo tukiomba atusikia na kutupa haja zetu. Somo katika Biblia, 1Yohana 3:22; Yohana 9:31; Methali 15:29. 

 SALA - Maana yake ni matukio yako ya kibinafsi mbele ya Mungu. Mahitaji ya lazima ni pamoja na mambo ya lazima kama vile chakula, mavazi, malazi na mengine yanayofanana na hayo, ndio maana Yesu anatoa mfano anavyosema sisi tunawapenda Watoto wetu vipawa vyema, pia anauliza ni nini hasa Baba wetu aliye Mbinguni atawapa mema wamwombao ?.. Vipawa vyema au mema ni maneno yanamaanisha hitaji au gharama tunayo mwomba Mungu. Soma katika Biblia,  Mathayo 7: 7-11.  

 MAOMBEZI - Ni jukumu lako la wengine au kuombea wengine badala ya kujihifadhi binafsi. Soma katika Biblia  1Wathesalonike 1: 2; 2; 11-12 na Wakolosai 1: 9. 

 SHUKRANI -  Ni neno la Kiebrania 'Yadah'  maana yake kusema maneno ya shukrani, Zaburi 107: 21-22; na Waebrania 13:15. Kushukuru ni jambo la muhimu sana mbele ya Mungu inatupasa kushukuru kwa kila jambo jema. Wale wakoma kumi waliotakaswa na Yesu kati yao alirudi mmoja kushukuru, wale tisa hawakuwa na moyo wa shukrani.Soma katika Biblia,  1Wathesalonike 5:18; Luka 17: 17-19.     

 KUABUDU - Linatokana na neon la Kiebrania ' Shachah', neno hili lina maana kuinama, kusujudia, au kwa kulala kifudifudi mbele za Mungu au chini ya miguu ya Mfalme. Soma katika Biblia,  Luka 4: 8; 2Samweli 24:20.  

 UPAKO -  Ni kumiminiwa mafuta, kutengwa au kuwekwa kwa ajili ya kazi maalum ya Mungu, kama ya ukuhani, ufalme na nabii. Soma katika Biblia.  Luka 4:18; 1Samweli 10: 1; 16:13; Kutoka 30:30; Ni kwamba mafuta, kumiminiwa mafuta, kutengwa au kuwako kwa sababu ya kazi maalum ya Mungu, kama ya ukuhani, ufalme na nabii. Soma katika Biblia. 
 Luka 4:18; 1Samweli 10: 1; 16:13; Kutoka 30:30; 1Wafalme 19: 15-16. 

Maoni

  1. MUNGU AWABARIKI SANA SANA WATUMISHI WA MUNGU

    JibuFuta
  2. Barikiwa mno imenisaidia

    JibuFuta
  3. Bila jina23:18

    Barikiwa Sana Mtumishi wa BWANA

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...