Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu wengine, kwa sababu hakuna mtu anayejua kila kitu au kila jambo na anayeweza kufanya kila kitu mwenyewe hapa duniani. Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Kwa sababu hiyo ili mtu apate msaada wa wengine ni lazima ajue namna ya kuishi na watu vizuri. Na ndipo ataishi kwa amani na watu wote. Zifuatazo ni kanuni muhimu za kuishi na watu. 1. Kuwapenda watu wote bila kubagua. Kwa sababu watu wote chanzo chake ni Mungu aliwaumba. Yeye ni Baba wa wote. Kwa sababu hiyo kila mtu ametokana na Mungu. 2. Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana. 3. Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake, hata akiwa ni masikini, hakuelimika, hana cheo cha juu na kadhalika. 4. Uwe mtu wa furaha katika Mungu siku zote. Kwa kulisoma neno lake, kuomba na kumsifu. 5 Uwe mtu unayesimamia neno la Mungu...
Kumjua Mungu kupitia maandiko matakatifu