Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MIUJIZA YA WATU KUANGUKA CHINI.




MIUJIZA YA WATU KUANGUKA CHINI

ASKOFU MKUU WA KANISA  LA FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP (F.G.B.F) TANZANIA.

ZACHARY KAKOBE

MHUBIRI WA KIMATAIFA, ASKOFU ZACHARY KAKOBE.
Tovuti       : WWW.bishopzacharykakobe.org

SOMO:  MIUJIZA YA WATU KUANGUKA CHINI

            Katika miaka ya hivi karibuni, kumezuka wimbi kubwa la miujiza ya “watu kuanguka chini”. Wimbi hili limezagaa sehemu nyingi duniani na hivi sasa, nchi yetu Tanzania imekubwa tayari na wimbi la “miujiza hii. Watu hawa wanaojiita watumishi wa Mungu, watasema kwa kiingereza, “RELEASE THE POWER OF GOD” wakimaanisha “NAFUNGULIA AU NAACHIA NGUVU YA MUNGU”, na baada ya kurusha mikono yao, au kupuliza hewa kwa mdomo, watu wataanguka chini kwa wingi wao, wakati mwingine kusanyiko zima, na watu watasema wameuona uwepo wa Mungu! Watu hawa wanafanya kile wanachokiita, “DEMONSTRATION S OF THE POWER OF GOD”, au “MAONYESHO YA NGUVU YA MUNGU”, huko na kule, na kuwaarika watu waje “kuona nguvu ya Mungu”. Kanisa la Mungu, lazima liwe macho. Hatupaswi kuwa watoto wachanga wa kiroho, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za uda nganyifu (WAEFESO 4:14 ). Kwa sababu hii, leo, tunachukua muda wa kutosha, kujifunza kwa undani juu ya mambo haya, ili Shetani asije akapata kutushinda kwa kukosa kuzijua fikra zake (2 WAKORINTHO 2:11 ). Tutaligawa somo hili katika vipengele saba:
( 1 ). UMUHIMU WA KUZIJARIBU ROHO.
( 2 ). JINSI YA KUZIJARIBU ROHO
( 3  ). MAKUSUDI YA MIUJIZA YA MUNGU.
( 4 ). MAFUNDISHO YANAYOTOKANA NA MIFANO YA      WATU KUANGUKA CHINI KATIKA BIBLIA.
( 5 ). JINSI YA KUKWEPA MADHARA YA ROHO  YA UPOTEVU.
( 6 ). JINSI YA KUMPA IBILISI NAFASI YA KUTUTUMIA.
( 7 ). JINSI YA KUWASAIDIA WALIOKUMBWA NA ROHO YA UPOTEVU.
( 1 ). UMUHIMU WA KUZIJARIBU ROHO.
          Ni muhimu kufahamu kwamba, siyo kila muujiza niwa Mungu, na siyo kila anayejiita Mtumishi wa Mungu, ni Mtumishi wa Mungu kweli. Shetani anaweza kufanya miujiza pia, kwa kutumia Watumishi wake, na wakawashangaza watu wengi, hata watu wengi wakawasikiliza na kusema, watu hawa ni uweza wa Mungu ule mkuu ( MATENDO 8:9-11; KUTOKA 7:8-11). Wakati wote, miujiza ya Shetani ina lengo la kuwapoteza kama yamkini au ikiwezekana, hata Wateule wa Mungu  ( MATHAYO 24:24 ). Ili Shetani afanikiwe kuwapoteza Wateule hatakuja kwetu kwa kuwatumia Wachawi au Waganga wa kienyeji. Akifanya hivyo tutashituka mapema. Atajigeuza awe mfano wa Malaika wa nuru, na Watumishi wake watajigeuza wawe mfano wa Watumishi wa haki ( 2 WAKORINTHO 11:13-15 ). Watumishi wake, watakuja kwetu wakishika Biblia na kuharibu Wokovu, ingawa hawatakuwa na msisitizo mkubwa kwenye Neno la Mungu na Utakatifu. Muda mfupi sana watautenga kwenye Neno la Mungu na muda muda mwingine utatumika kufanya maonesho ya “miujiza” yao. Ndiyo maana ni muhimu sana kuzijaribu roho na kutokuamini kila roho ( 1YOHANA 4:1 ). Roho zote zinazotokana na Mungu, ziko chini ya Roho wa Kweli, Roho Mtakatifu, na roho zote zinazotokana na Shetani ziko chini yaROHO YA UPOTEVU, Shetani mwenyewe ( 1YOHANA 4:6 ). Chochote kinachofanyka lazima tukijaribu na kujua kwamba kiko kundi lipi kati ya hayo mawili ( 1WATHESALONIKE 5:21 ).
( 2 ). JINSI YA KUZIJARIBU ROHO.
           Tutawezaje kuzijaribu  roho hizi na kufahamu kwamba zinatokana na Mungu au la? Jinsi ya kuzijaribu, SIYO KUOMBA WALA KUFUNGA, bali tunazijaribu kwa NENO LA MUNGU! Roho zinazotokana na Mungu, ziko chini ya ROHO WA KWELI. Neno la Mungu,ndiyo KWELI ( YOHANA 17:17 ). Neno la Mungu ndiyo taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu. Kwa kutumia taa na mwanga huu, tunamulika na kuona vitu vya hatari na kuviepuka! Roho ya upotevu, haiendani na Kweli ya Neno la Mungu ( YOHANA 8:44-47 ). Roho ya upotevu hupotosha tafsiri ya Neno la Mungu na kulitumia isivyo ( MATHAYO 4:5-7; ZABURI 91:10-12 ). Tuchukue muda basi kuiangalia tafsiri ya kweli ya Neno la Mungu kuhusu miujiza.
( 3 ). MAKUSUDI YA MIUJIZA YA MUNGU.
           Miujiza ya Mungu wakati wote, hufanyka iliKULIONDOA TATIZO na kamwe haifanyiki kamaMAONYESHO YA NGUVU YA MUNGU! Miujiza yote ya Mun gu kwa mkono wa Musa, katika nchi ya Misri, ilikuwa na lengo la kumfanya Farao awaachie wana wa Israeli na kuacha kuwatumikisha; miujiza hiyo haikufanywa kama maonyesho ya nguvu ya Mungu! Musa aliponyoosha Fimbo yake juu ya Bahari ya Shamu na kuigawanya, muujiza huo ulikuwa na lengo la kuondoa tatizo, siyo “SHOW”! Maji machungu ya Mara yalipogeuzwa kuwa matamu, haikuwa “SHOW” au onyesho! Bwana alipoleta “Mana” kutoka Mbingu au Kwale, miujiza hiyo haikuwa “show” ilikuwa na lengo la kuondoa matatizo. Jua liliposimama kimya na likachelewa kuchwa  kama muda wa siku nzima wakati wa Yoshua, muujiza huo haukuwa onyesho la nguvu za mungu   bali lilikuwqa na lengo la kuondoa  tatizo la kukosa mwanga wakati wa vita. Jaribu kutaja kila muujiza! Danieli kukaa pamoja na simba katika tundu, haikuwa “SHOW”! Shadraka na Meshaki na Abedinego walipotupwa kwenye moto wasiteketee, muujiza huo haukuwa onyesho ya nguvu ya Mungu bali kulikuwa na tatizo la kuondoa. Yesu alipobadili maji yakawa divai, muujiza huo haukuwa onyesho ya nguvu ya Mungu bali walikuwepo watu waliokuwa na tatizo la kutindikiwa divai wakati wa harusi. SHETANI NDIYE MFANYA MAONYESHO(MATHAYO 4:8). Mazingaombwe ni maonyesho ya Shetani! Mungu hafanyi maonyesho ya nguvu yake ili kutafuta watu wamwamini. Yeye anadumu wa kuaminiwa hata kama hatutamwamini ni kwa kungoja afanye maonyesho ( 2TIMOTHEO 2:12-13 ). Mafarisayo na Masadukayo walipomuomba YesuAWAONYESHE ishara itokayo Mbinguni, hakuwapa ishara, aliwaacha akaenda zake! ( MATHAYO 16:4 ). Je, alipowaacha walionekana hana nguvu ya Mungu? Yeye hudumu wa kuaminiwa. Miujiza ya Mungu hutumika kutuondolea mizigo yetu na kutufanya tumwamini kuhusiana na upendo wake,huruma zake, ahadi zake n.k. Watu wakisema watuombee ili twende Mbinguni kutalii na kurudi, huyu siye mungu wa Biblia, ni mungu wa dunia hii, baba wa uongo, Ibilisi.
( 4 ). MAFUNDISHO YANAYOTOKANA NA MIFANO YA WATU  KUANGUKA CHINI KATIKA BIBLIA.
          Mahali pote katika Biblia tunapoona watu wasio na mapepo wakianguka chini mbele ya utukufu wa Mungu, hakukuwa na mikutano ya Injili, wala watu wa kuwaombea na kuanguka wenyewe, na kulikuwa na kusudi au sababu, aidha walianguka na kuwekwa tayari kuisikia sauti ya Mungu, wengine walianguka wenyewe kwa hofu au kwa hiari yao ili wamuombe Mungu au kumsihi Yesu awaponye n.k.Kamwe, kuanguka kwao hakukutokana na onyesho la nguvu ya Mungu au maombezi ya mtu yeyote.. ( MIFANO: EZEKIELI 1:8; 3:22-23; 43:1-7; 44:4-5; MATHAYO 17:1-8; 26:38-39; LUKA 5:12-13; YOHANA 18:2-6; MATENDO 9:1-6; 26:12-18; 16:26-30 ). Watu pekee walioanguka chini baada ya mtumishi wa Mungu kufanya maombezi, walikuwa ni watu wenye mapepo.. Mapepo ndiyo yaliyokuwa yanaanguka ( LUKA 8:26-29; MARKO 3:11 ). Iweje basi kwa watu hawa kwamba KILA MTU katika mikutano yao, sharti aanguke chini, hata kama anataka kutoka kwa Mungu, kazi, fedha, kurudiana na mumewe, kushinda mitihani, chumba cha kupanga, mchumba n.k? La kushangaza ni kwamba wengi huanguka chini na matatizo na kuinuka wakiwa na matatizo hayohayo! Ni Mungu yupi huyo!
( 5 ). JINSI YA KUKWEPA MADHARA YA ROHO YA UPOTEVU.
           Kama tulivyojifunza, roho ya upotevu inajaribiwa kwa Neno la Mungu. Yesu alimshinda Shetani kwa IMEANDIKWA NA TENA IMEANDIKWA! ( MATHAYO 4:4-11 ). Neno la Mungu ni upanga wa Roho wa kumshindia adui Ibilisi ( WAEFESO 6:17 ; WAEBRANIA 4:12-13 ). Kwa sababu hii baada ya kuokoka hatupaswi kukimbizana na mikutano ya Injili huku na kule na kutafuta misisimuko tu bali tutafute na kutulia mahali tunapoweza kujifunza Neno la Mungu kipengele kwa kipengele, amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, huku kidogo na huku kidogo katika Biblia nzima ( ISAYA 28:9-10 ).
( 6 ). JINSI YA KUMPA IBILISI NAFASI YA KUTUTUMIA
Watu wengi wanaotumiwa na Shetani kufanya miujiza hii, wamempa Ibilisi nafasi kuwatumia ingawa hapo mwanzo wengi wao walikuwa watoto wa Mungu hasa. Wamempa Ibilisi kwa jinsi ifuatavyo:-
  1. KUTAKA KARAMA ZA MUNGU BILA UTAKATIFU-Njia iliyo bara ya kutaka karama zilizo kuu, ni kutafuta KWANZA upendo wa ki-Mungu ulio mbali na kiburi, majivuno, kukosa adabu, kufurahia udharimu n.k. Upendo hufurahia pamoja na KWELI. Ni utakatifu ( 1 WAKORINTHO 12:28-31 ). Karama za Mungu ni za Roho MTAKATIFU, hivyo  hutenda kazi kikamilifu katika utakatifu. Kutaka karama bila kutaka utakatifu, na kutaka kutumiwa na Shetani!
  2. KUWA RAFIKI WA DUNIAUkiwa rafiki wa dunia yaani kuwa sawa na watu wa dunia katika kusema, kuvaa, kutenda n.k, unakuwa ADUI wa Mungu. Hawezi kukutumia. Atakutumia Ibilisi ( YAKOBO 4:4 ).
  3. KUWA NA KIBURI NA KUKATAA USHAURI– Wengi wao Roho Mtakatifu amewaonya kwa njia mbalimbali na pia akiwatumia wat wa Mungu kuwaeleza kuwa huduma hiyo siyo ya Mungu, lakini kwa kiburi wamedhani wanaonewa wivu wakaendelea ( METHALI 11:2; YEREMIA 50:31-32; METHALI 16:18; 11:14; 19:20; 20:18 )
( 7 ). JINSI YA KUWASAIDIA WALIOKUMBWA NA ROHO YA UPOTEVU..
          Tuwarejeze upya kwa roho ya upole huku tukijiangalia nafsi zetu wenyewe tusijaribiwe kama wao na pia kuwaombea ( WAGALATIA 6:1; 1YOHANA 5:14-16; YAKOBO 5:16 ). Kuna Baraka tele kufanya hivi ( YAKOBO 5:19-20 ).
SOMOJE, KUCHEZA AU KUSHABIKIA MPIRA NI DHAMBI? Ingia hapahttps://davidcarol719.wordpress.com/je-kucheza-au-kushabikia-mpira-ni-dhambi/
OMBI LANGU KWAKO.
         Share ujumbe huu na  marafiki zako wa “facebook” na “twitter” kwa kubonyeza kitufe chenye neno “share” hapa chini ya maneno haya. Ukifanya hivyo, utakuwa mmoja kati ya maelfu ya watu wengine watakaopokea baraka za Mungu kwa kusambaza somo hili kwa maelfu ya watu katika mitandao mbalimbali ya internet.
MUNGU AKUBARIKI SANA!!

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...