Ninayo furaha kwa ajili ya wakati huu ambao Mungu amenijalia kufundisha neno lake. Ni wakati muhimu wa kujifunza neno la Mungu ambalo ni habari njema inayotujenga katika imani. Kwa hiyo tunajegwa na kuwa imara katika kumtumikia Mungu.
Kwa sababu hiyo ili watumishi wa Mungu wajengwe na kuwa imara katika neno la Mungu wanapaswa kujifunza kwa bidii. Jambo lingine wanapaswa kujifunza kwa watumishi wengine wanapokuwa wanafundisha au kuhubiri neno la Mungu.
Ikiwa mtumishi wa Mungu anajihesabia haki ya kwamba anajua mambo yote ya Mungu Si sahihi, bali anajidanganya nafasi yake mwenyewe. Lakini tunaweza kuyafahamu maneno ya Mungu katika ukamilifu wote. Ila hatuwezi kuyafahamu mambo yote ya Mungu kwa sababu si yote ametufunulia. Ndio maana Imeandikwa;
“Mambo siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.” Kumbukumbu Torati 29:29. “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu;...” 1 Wakorintho 13:9.
“Mambo siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.” Kumbukumbu Torati 29:29. “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu;...” 1 Wakorintho 13:9.
Tunaweza kuona habari njema ya wokovu ilikuwa imefichwa, lakini kwa pendo lake Mungu aliwafunulia manabii na mitume. Kwa sababu hiyo wakaweza kuihubiri siri ya Mungu kwa mataifa yote. Ndio maana mtume Paulo alisema; “Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele,” Warumi 16:25. “pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;”
Waefeso 6:19.
Kwa sababu hiyo kuna mambo ambayo yamefichwa katika neno la Mungu. Ikiwa mwalimu au mhubiri anayo bidii ya kujifunza yeye mwenyewe na kwa watumishi wengine atakuwa amejifunza jambo jipya. Kwa hiyo kwa kadri anavyojifunza anazidi kuyafahamu mambo ya Mungu.
Jambo la muhimu kuzingatia tambua ya kwamba Mungu hufunua mambo yaliyofichwa katika neno lake kwa wale wote wampendao. “Siri ya BWANA iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.” Zaburi 25:14. “Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa BWANA, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.” Mithali 3:32.
Mwalimu au mhubiri wa kweli anapaswa kuwa mfano kwa wengine kama ifuatavyo;
1.Ni muhimu aishi neno la Mungu linavyosema.
2. Awezaye kufundisha na kuhubiri kwa usahihi neno la Mungu.
3. Awezaye kuomba sawasawa na neno la Mungu.
4. Mazungumzo yake ni lazima yaendane na neno la Mungu.
5. Anayefaa mavazi vyenye staha (heshima).
Maoni
Chapisha Maoni