Ruka hadi kwenye maudhui makuu

USHAURI HULETA WOKOVU.

Karibu katika somo hili ambalo ni muhimu kwa ajili ya kila mtu. Kabla ya kuendelea na somo hili linalohusu ”ushauri huleta wokovu” nitatoa mfano ili uweze kuelewa zaidi.  Kila mwanadamu ambaye Mungu alimuumba hawezi kufahamu mambo yote. Pia hawezi kufanya kila jambo. Ndio maana tunaweza kuona ya kwamba, kuna watu wenye elimu ya ujuzi tofauti na mwingine. Twaweza kuona kuna  mainjinia wa ndege, magari, meli na nyumba. Kuhusu afya ya mtu na matibabu, kuna nadaktari na wauguzi. Kwa hiyo tunaweza kuona makundi hayo yote yanatofautiana katika utendaji wa kazi. Lakini makundi hayo yanajenga na kuboresha maendeleo ya jamii ulimwenguni kote.

Kwa upande wa kanisa Mungu amelijali Karama kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo. Kwa sababu hiyo kila mkristo anayo Karama ya  pekee ambayo amepewa kwa ajili ya kanisa. Kwa hiyo unaweza kuona kila mkristo ni muhimu kwa mwingine. Hakuna mtu yeyote anayeweza kujitegemea katika mambo yote bila kuhitaji msaada kutoka kwa mtu mwengine. Kwa sababu hiyo ndani ya kanisa kuna viungo vingi kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo. Kwa hiyo kila kiungo kina kazi ya pekee tofauti na viungo vingine. Kwa hiyo ndani ya kanisa kuna wakristo ambao wamejaliwa kuwa na karama ya ushauri wa mambo ya Mungu.

Ni muhimu kufahamu watu ambao ni sahihi wanaoweza kukushauri  katika jambo lako. Ni
kama ifuatavyo;
1.Watoto wanaweza kuwashauri  wazazi au walezi wao kuhusu jambo fulani. Haijalishi ya kwamba wana umri gani, lakini wanaweza kutoa ushauri wenye maana na kutatua jambo.

2.Watu ambao ni wa kawaida wanaweza kuwashauri wengine wakiwemo viongozi mbalimbali. Inawezekana ikawa ni watu wenye elimu au hawana elimu. Lakini ushauri wao ni mahususi kwa ajili ya kutatua jambo ambalo lipo.

3. Watu walio waaminifu na kutunza siri. Ninasema hivyo kwa sababu pengine jambo lako ni la siri au sio la siri lakini usingependa lijulikane kwa watu wengine. “Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. Mithali 11:13”

4.Watu wenye ufahamu na hekima ya mambo mbalimbali. Hao ndio wanaoweza kukupa ushauri unaofaa. Tukiangalia maeneo ambayo mwanadamu anahitaji msaada ni mengi sana. Ila hapa nitataja machache; ambayo ni kuhusu biashara, kampuni, kilimo, kuoa au kuolewa, maisha ya ndoa, kulea watoto na maisha ya mwanafunzi katika elimu.

Ni jambo la muhimu kila mtu kutambua ushauri huleta wokovu katika maisha ya mtu, familia, jamii na viongozi mbalimbali.
“Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu. Mithali 11:14” “Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu. Mithali 24:6

Asiyetaka kushauriwa anaweza kusababisha madhara katika maisha yake. Pia anaweza kusababisha madhara kwa wengine; kama, familia, jamii na taifa lote.

Tahadhari kuhusu ushauri.
Kuwa makini kuhusu ushauri ambao unakuwa umepewa. Jambo la kwanza fahamu si kila ushauri unaopewa ni sahihi. Kuna ushauri wa aina mbili  kama ifuatavyo;
1.Ushauri mzuri.
Musa alipewa ushauri mzuri na mkwewe Yethro ili achague watu ambao watakuwa wanamsaidia kufanya kazi ya Mungu. Kwa sababu kazi ya Mungu ilikuwa kubwa aliifanya kuanzia asubuhi hadi jioni kila siku, wala hakupata muda wa kupumzika. Ndio maana mkwewe Yethro alimshauri Musa achague watu ambao watamsaidia kufanya kazi ya Mungu.
“Asubuhi yake Musa akaketi ili awapishie hukumu watu; na hao watu wakasimama kumzunguka Musa tangu asubuhi hata jioni. Mkwewe Musa akamwambia, Jambo hili ufanyalo si jema. Huna budi utadhoofika wewe, na hawa watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako. Nawe utawafundisha zile amri na sheria, nawe utawaonyesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo inawapasa kuifanya. Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi; nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe. Kutoka 18:13,17-18,20-22”

2.Ushauri mbaya.
Mfalme Rehoboamu alikuwa ameomba ushauri kwa wazee na vijana ili awape jibu wana wa Israel, ambao walikuwa wamemwomba awapunguzie utumwa mgumu. Wazee walimpa ushauri mzuri, lakini vijana walimpa ushauri mbaya ambao aliwapa Wana Wa Israeli. Kwa hiyo ni muhimu kupima ushauri unaopewa na kutambua ni ushauri upi unaofaa na kuufanyia kazi. “Wakapeleka ujumbe, wakamwita, Yeroboamu akaja na Israeli wote, wakamwambia Rehoboamu, wakasema,Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa upunguze utumwa mgumu wa baba yako, na kongwa lake zito alilotutwika, nasi tutakutumikia.
Akawaambia, Mnirudie baada ya siku tatu. Watu wakaenda zao. Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake, alipokuwa hai bado, akasema, Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa? Wakamwambia, wakasema, Ukiwa mwema kwao watu hawa, na kuwapendeza, na kuwaambia maneno mazuri, ndipo watakapokuwa watumishi wako siku zote.
Lakini akaliacha shauri lile la wazee walilompa, akataka shauri kwa wale vijana waliokua pamoja naye, waliosimama mbele yake.
Akawaambia, Je! Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakisema, Utufanyie jepesi kongwa alilotutwika baba yako.
Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliosema nawe, wakinena, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, lakini wewe tufanyie jepesi; uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu akiwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge. Basi Yeroboamu na watu wote wakamjia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu. Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee,  nao kwa shauri la vijana, 2 Mambo ya Nyakati 10:3-13”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...