Yesu alifundisha ya kwamba yatupasa tuwe wakamilifu kama Baba yetu wa Mbinguni alivyo mkamilifu. Huku akiwa ameonyesha wazi upendo wa Mungu kwa wanadamu, jinsi Mungu anavyowatendea wema wenye haki na wasio haki. Kwa sababu hiyo yatupasa kutenda kama Mungu kwa kuonyesha
upendo wetu kwa watu wote.
Je? Tunawezaje kuonyesha upendo wa Mungu kwa jinsi gani? Jibu la swali hili ni kama ifuatavyo:
1. Kuwapenda watu wote.
2. Kuwatendea mema watu wote.
3, kuwaombea baraka watu wote.
Kamwe! Hatuwezi kumpendeza Mungu kama tunawatakia adui zetu wapatwe na mabaya. Pia hatupaswi kuwaombea maadui zetu ili wapatwe na mabaya. , Hayo siyo mapenzi ya Mungu kwetu. Mapenzi ya Mungu katika maandiko yanasema; "Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.” Mathayo 5:43-48.“Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.” Warumi 12:14.
Kwa hiyo kutokana na somo hili mkristo ambaye ameokoka ili aweze kuwa mkamilifu yampasa kuyatenda yale yote ambayo Mungu ameagiza katika sheria yake. Kwa sababu hiyo anakuwa ni mtakatifu kama Mungu alivyo mtakatifu.
Tunaweza kuona ya kwamba hakuna viwango vya ukamilifu na Utakatifu. Kiwango ni kimoja tu ambacho ni kuwa mkamilifu na mtakatifu kama Mungu alivyo. Inamaana yatupasa kuwa na utakatifu wa Mungu. Au kwa maelezo mengine kuwa sawa na Mungu katika utakatifu. Ndio maana amesema hivi;
“Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.” Walawi 20:26. “kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” 1 Petro 1:16. Kwa hiyo andiko hili hapa juu linaonyesha wazi ya kwamba mtu atakuwa ametengwa na kuwa mali ya Mungu iwapo atakuwa ni mtakatifu kama Mungu alivyo mtakatifu. Kwa sababu hiyo ikiwa kuna mtu anadhani hakuna mwanadamu anayeweza kuwa mkamilifu na mtakatifu huyo hayajui maandiko kwa ukamilifu. Ingekuwa ni jambo ambalo haliwezekani kwa mwanadamu kutimiza Mungu asingetoa agizo watu wake wawe watakatifu. Na pia asingesema “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.” Zaburi 16:3. Pia andiko lingine linathibitisha na kuonyesha ya kwamba mwanadamu anaweza kuishi maisha ya utakatifu. Ikiwa ameweka nia moyoni kuzishika amri. Ndio maana imeandikwa;
Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. 1 Yohana 5:3Jambo lingine ambalo si sahihi ikiwa mtu anafikiri ya kwamba mkristo anapookoka anakuwa ni mchanga na bado anatenda dhambi siyo kweli. Kwa sababu mtu anapozaliwa kwa mara ya pili anakuwa ameamua kuachana na dhambi na kuungama na kuwa kiumbe kipya. Pia anakuwa ni mkamilifu na mtakatifu kama Baba yetu wa mbinguni alivyo. Mkristo anapookoka anakuwa ni mchanga kwa sababu bado hayajui sana maneno ya Mungu. Ila anakuwa ameyafahamu maneno ya Mungu kwa sehemu ndio maana akaokoka. Ukiangalia kwa makini katika neno la Mungu limeweka wazi jambo hili; ndio maana imeandikwa, “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” 2 Wakorintho 5:17. “Ila sasa ninakwenda Yerusalemu, nikiwahudumu watakatifu;”
Warumi 15:25. Mtumishi wa Mungu mtume Paulo alithibitisha ya kwamba kanisa la Yerusalemu ni watakatifu. Pia alithibitisha na makanisa mengine yaliyokuwa sehemu mbalimbali vilevile walikuwa ni watakatifu. Alikuwa na maana ya kwamba wakristo waliookoka siku za karibu na wale wa waliookoka tangu siku nyingi wote ni watakatifu.
Hapa nitaelezea kuhusu wakristo wachanga na wale walioukulia wokovu.
“Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.” Waebrania 5:12-14. Kutokana na maandiko hayo yanaonyesha makundi mawili ya wakristo waliookoka ambao ni kama watoto wachanga na watu wazima.
Mtoto mchanga ni mkristo ambaye ameokoka lakini bado hajakuzwa kwa ukamilifu kwa mafundisho ya awali au ya kwanza ya neno la Mungu.
Na mtu mzima ni mkristo aliyeokoka na kufundishwa mafundisho ya kwanza na kuukulia wokovu. Kwa sababu hiyo kwa kadiri anavyoendelea kufundishwa neno la Mungu anakuwa amepewa chakula cha watu wazima.
Ili mtu aliyeokoka aweze kudumu katika ukamilifu na utakatifu ni lazima azingatie haya yafuatayo;
1 Yampasa kutawala moyo wake asiwaze mabaya wala kutamani mambo yasiyofaa.
2. Yampasa kutawala kinyme chake asije akasema maneno yasiyofaa. Andiko linasema, “... Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu. Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.” Yakobo 3:2,6. Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. 1 Wakorintho 15:33.
Kipimo cha utakatifu.
Kama mkristo atapima utakatifu wake kwa miujiza anayoifanya au kwa kunena kwa lugha mpya hiyo siyo njia sahihi.
Mkristo anaweza kuuthibitisha utakatifu wake kwa njia zifuatazo;
1. Ikiwa anaishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema.
2. Ikiwa ameziungama dhambi
zote na kusamehewa.
3. Anaishi maisha yasiyo na
dhambi yoyote.
Kwa sababu hiyo akiwa mtu amethibitisha utakatifu alio nao kupitia njia hizi hapa juu ndipo anakuwa na uhakika ya kwamba yeye ni mtakatifu. Naye Roho mtakatifu humshuhudia nafsni mwake.
Sasa unaweza kubofya hapa chini na kuendelea na soma linalosema; KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.
Kwa sababu hiyo akiwa mtu amethibitisha utakatifu alio nao kupitia njia hizi hapa juu ndipo anakuwa na uhakika ya kwamba yeye ni mtakatifu. Naye Roho mtakatifu humshuhudia nafsni mwake.
Sasa unaweza kubofya hapa chini na kuendelea na soma linalosema; KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.
Maoni
Chapisha Maoni