Ninaposema utukufu wa Mungu hushuka ni kweli. Tunaweza kuona na kudhibitisha katika maandiko ya kwamba Mungu wakati wa Agano la kale alidhihirisha uwepo wake aliposhuka katika wingu hekaluni. "Hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa BWANA". 2 Mambo ya Nyakati 5:14. Pia nyakati hizi za Agano jipya Mungu anadhihirisha uwepo wake katika Roho Mtakatifu wakati anaposhuka juu ya kanisa.
Kwa hiyo ni muhimu watumishi wa Mungu kuwa makini na kutambua uwepo wa Mungu unaposhuka. Ili kuacha nafasi ya ya kanisa kububujika katika Roho Mtakatifu bila kuwanyamazisha. Huo ni muda wa peke kwa kila mtu kujimimina kwa maomba, sifa na shukrani mbele za Mungu.
Kwa hiyo si vyema mtumishi wa Mungu kuwanyamazisha waamini wakati Roho Mtakatifu anaposhuka juu yao. Kwa hiyo kufanya hivyo ni kumzimisha na kumzuia nafasi ya kutenda kazi katika wakatifu.
"Msimzimishe Roho;
msitweze unabii;
jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; 1 Wathesalonike 5:19-21."
"Msimzimishe Roho;
msitweze unabii;
jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; 1 Wathesalonike 5:19-21."
Uwepo wa Roho Mtakatifu unaposhuka juu ya watakatifu hudumu kwa muda wa dakika chache. Huo ni wakati ambao Mungu hukutana na watoto wake na kuwasaida. Pia huo ni wakati mzuri ambao watakatifu hupeleka sifa na maombi mbele za Mungu.
Maoni
Chapisha Maoni