Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MTU ANAVYOWEZA KUPOTEZA IMAINI.

Ninafundisha mambo ambayo ni sababu kwa  mkristo aliyeokoka kupoteza imani yake. Tutaangalia matokeo yatokanayo kwa mkristo ambaye amepoteza imani. Ni kama ifuatavyo;

1. Anakuwa amepoteza ujasiri wa Mungu ndani yake. Kwa sababu hiyo anakuwa na hofu na mashaka. Hali ya kutoamini inachukua nafasi moyoni mwake. Tunaweza kuona  na kujifunza kwa Yesu Kristo alivyowafundisha wale mitume wake.Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Marko 11:22-23.”
2. Jambo lingine mkristo anapokuwa amepoteza imani anakuwa hana matumaini kwa Mungu.

Mambo ambayo ni sababu ya mtu kupoteza imani yake;  Ni haya yafuatayo.
1.Kuishi katika dhambi.
2. Kuwa na mashaka.
Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote. Yakobo 1:6-8.”

Ni muhimu kutambua kusudi la Mungu kwetu, alipotuumba aliweka kanuni mojawapo ambayo ni kuishi kwa imani kwa kumtumaini Mungu. Pia kuishi maisha ya haki. Mtu anaweza kuishi maisha ya haki kwa kuyatenda mambo yote sawasawa na neno la Mungu. Kwa sababu hiyo humpendeza Mungu kama ilivyoandikwa; Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu. Waebrania 10:38-39.” Kuna jambo la kujifunza kutokana na huu msitari hapa juu. Unaonesha ikiwa mtu anashindwa kumtumaini Mungu na kumtegemea na kusta sita atapotea. Ina maana atahukumiwa na kutupwa Jehanum ya moto na kuteseka milele. Hata hivyo katika kitabu cha Waebrania Jambo hilo limeandikiwa. Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi? Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. Waebrania 3:18-19.”

Mambo ya kuzingatia ili kujengwa,kuimarishwa na kudumu katika imani ni haya yafuatayo;
1.Kujifunza neno la Mungu kwa bidii na kujengwa katika imani.
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Warumi 10:17.”
2 .Kuyaweka maneno ya Mungu moyoni mwako. Ukifanya hivyo ni rahisi kutambua mambo yoyote ambayo ni kinyume na neno la Mungu na kuyaepuka. Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,
Nisije nikakutenda dhambi. Zaburi 119:11.”
3. Kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. Zaburi 119:9.

4. Kuishi kwa kumtumaini na kumtegemea Mungu katika mambo yote.Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu,
Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. Zaburi 125:1-2.”  Kutokana na andiko hilo linaonesha ya kwamba mtu anayemtumaini Bwana atakuwa imara na kulindwa na yeye.
5.  Kuomba na kufunga. Ni jambo la muhimu sana na kuzingatia kwa sababu kuna mambo ambayo hayawezekani ila kwa kuomba na kufunga.

Ndio maana Bwana wetu Yesu Kristo kabla ya kufanya huduma ya kuhubiri habari njema na kufanya matendo makuu kuna mambo ya kwanza ambayo yangefanyika kwake ni kama ifuatavyo;
•Alibatizwa.
•Alijazwa Roho Mtakatifu.
•Aliongozwa na Roho kufunga.
Baada ya hayo ndipo alianza kuhubiri na kutenda matendo makuu ya Mungu. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...