Hivi sasa ni nyakati za mwisho na yule mwovu amekuwa na wivu kwa ajili ya wale ambao wamesimama imara na kumtumikia Mungu. Kwa sababu hiyo halali usingizi anafanya bidii mchana na usiku ili amwangushe mmojawapo. “ Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. 1Petro 5:8.” Kwa hiyo kila mkristo aliyeokoka na kusimama imara yampasa kuwa makini asije akayaamini mafundisho na mahubiri ya uongo na kupotea. Nyakati hizi kuna baadhi ya watu ambao wanafundisha na kuhubiri kwa kupotosha neno la Mungu katika biblia. Wanayoyafundisha tunaweza kuyambua kwa sababu yako kinyume na maandiko. Kwa hiyo ukiyalinganisha na maandiko katika biblia hayaendani, bali yanapingana. Njia nyingine ya kuwatambua waalimu wa uongo ni kupitia maisha wanayoishi ambayo ni kinyume na neno la Mungu. “ Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala m...
Blogu hii imekuwa msaada kwa watu wengi. Wamelifahamu neno la Mungu na kuimarika katika kumjua Mungu. Washirikishe na wengine.