Ruka hadi kwenye maudhui makuu

WASHINDI WATAURITHI UFALME WA MUNGU.

Watoto wa Mungu ambao wamezaliwa mara ya pili watakuwa wanakutana na mitihani ya majaribu. Kwa hiyo  mkristo ambaye ataweza kushinda majaribu na kuingia mbinguni ni yule ambaye atazingatia mambo haya yafuatayo;

1. Kuutafuta uso wa Mungu kwa Bidii kila wakati kwa maombi na kufunga.

2. Kuutafuta uso wa Mungu kwa kujifunza neno lake kwa bidii na kulifahamu.

4. Kudumu kwa kuishi neno la Mungu linavyosema na katika utakatifu. "
Ufunuo wa Yohana 3:4-5  
Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake."

5. Kulisimamia neno la Mungu kwa usahihi. Wala usilionee aibu neno la Mungu mbele za watu na kushiriki kufanya mambo yao ambayo ni kinyume na neno la Mungu. Yakupasa kukataa kufanya mambo ambayo ni kinyume na neno la Mungu."
1 Timotheo 5:22

"...wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi. 2 Wakorintho 6:17-18
Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.

6.Kuyatafakari mambo ya Mungu katika maisha yetu. Hayo ndiyo aliyotuitia kwa ajili ya ufalme wake. Mtu anaweza kutafakari neno la Mungu na matendo mema ambayo Mungu amemtendea. Pia kutafakari Mamlaka na kuu wake usiopimika. "Wakolosai 3:1-2 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi." 
"Zaburi 119:97
Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa." 
"Zaburi 63:6 Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari Wewe8 makesha yote ya usiku."
Mkristo ambaye anamtafakari
Mungu kinywa chake hakitapungua sifa na shukrani kwa Mungu. watu wote ambao wamemwishia Mungu hao ndiyo washindi watakaoingia mbinguni. Mbinguni ni mahali pazuri na patakatifu. Hayo ni makao ya kuishi watakatifu kwa amani na furaha  milele. Dhiki na shida za dunia hii zitakuwa zimepita. "Ufunuo 21:1-5

Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya....Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika nacho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita ....Tazama nayafanya yote kuwa mapya....".

Wewe ambaye utakuwa umelisoma somo hili ni muhimu ukafahumu Mungu amekupa nafasi ya kuishi hapa duniani mara moja tu. Hapa duniani siyo mahali ambapo mwanadamu ataishi milele. Sisi wote ni kama wasafiri lakini baadae hatupo katika ulimwengu huu wa sasa. 1 Petro 1:24
Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka; Waebrania 9:27
Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; Andiko hili limeonyesha wazi mtu akifa kwa wakati huo huo anakuwa amekwisha hukumiwa.  Kwa sababu hiyo kwa mkristo aliyeokoka yampasa kudumu katika ushindi na kuutunza. Ufunuo wa Yohana 3:11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. Mtu
 akifa katika dhambi hana nafasi nyingine ya kurudi duniani ili atubu. Ninamalizia kwa kusema mwanadamu amewekewa kuzaliwa mara moja, kuishi mara moja na kufa mara moja. Kwa hiyo nafasi hii uliyopewa ya kuishi ni muhimu kuitumia ukiwa tayari kwa ajili ya kuingia ufalme wa Mungu. Siku ile nitakapokuona mbinguni kwa Baba nitafurahi sana.

Maoni

  1. Bila jina20:17

    Nina mtukuza Sana Mungu wa Mbinguni kwaajili ya kazi yenu nzur na iliyo tukuka.. Nikwel mnafanya kaz . Aliyo waagiza Bwana Yesu.. Kwamba Enenden ulimwenguni kote Mkahubir Injili. Kwa kila kiumbe na kila Aaminie na kubatizwa Huyo ataokoka... Ni maombi yangu kwa Mungu Awatunze mnoo . Na uweza wake ukawe juu yenu Ameen.🙏🙏🙏

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...