![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg-SGgKxXByhSBTjVFugwPEWDK8A4LP6-WBzzathNOLNhPnLQeFWE68peezhygnlB4dLr9hAtslUeD8x43_d-PVDlVPYgcbC5C_U76F-2fdmlfw4i6BUkTXdvC1yvtkk4kkYFP2pF0Vtkps/s320/VIPIMO.jpg)
Maana ya vipimo vya haki ni vipimo vyenye uwiano ulio sawa. Kwa mfano mizani ni kipimo chenye uwiano ulio sawa. Vipimo ambavyo siyo rasmi ambavyo jamii inavitumia kupimia bidhaa kama ndoo, magunia, nakadhalika. Vipimo hivyo ikiwa mtu anavitumia kwa namna isiyo sawa humpunja mnunuzi au muuzaji. Baadhi ya wanunuzi wanapokwenda kununua mazao kama viazi au vituguu wanataka gunia lijazwe kupita ujazo unaotakiwa hivyo hushonea ziada wanayoiita LUMBESA.
Kwa mfanya biashara yampasa kuuza bidhaa zake sawasawa na bei ya sako. Ikiwa mtu anauza kitu chochote pia yampasa kuuza bei ya soko. Kwa sababu hiyo anakuwa ameuza kwa bei ya haki.
Lakini kwa mtu yule auzaye kitu au bidhaa yoyote kinyume na bei ya soko anakuwa amelangua au kwa neno lingine ni mlanguzi. Hapa nitatoa mfano ili uweze kuelewa zaidi. Ikiwa kitu kinauzwa kwa bei ya soko ambayo ni Sh. 20, lakini ukakiuza kwa shilingi 25 au kwa shilingi 30 unakuwa umeuza kwa bei isiyo ya haki. Kufanya hivyo siyo haki mbele ya Mungu, kwa kuwa Mungu amesema:
"Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. Kwa kuwa wote wayatendayo mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako. Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo.” Kumbukumbu 25:15-16.
“Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana;zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.” Mithali 3:1-2
Kutokana na neno la Mungu hapa juu linaonyesha wazi ya kwamba mtu akitenda haki na kuishi sawasawa na sheria na amri za Mungu ataongezewa miaka nyingi ya kuishi hapa duniani. Ina maana ya kwamba hatakufa mapema kwa sababu amemtii Mungu kwa kutenda Sheria na amri zake. Pia atamjalia kuishi kwa amani.
Hapa nitaelezea maana ya neno Mlanguzi. Ni kama ifuatavyo;
1.Ni mtu anayenunua bidhaa, kutoka kwa wakulima, kwa bei rahisi na kuwauzia wengine kwa bei ghali ili kupata faida kubwa.
2.Mfanyabiashara wa mnadani.
3.Mtu anayefanya biashara isiyo halali.
Maoni
Chapisha Maoni