Mambo ya kuzingatia ili uweze kuwa huru kutoka pepo wabaya ni haya yafuatayo:
(1) Mtu ni lazima awe ndani ya Kristo. (2) Kuishi neno la Mungu linavyosemaNdio maana Yesu waliwaambia wale wanafunzi wake "Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.” Yohana 15:3. Mtu aliye safi pepo hawana nafasi kwake, wala hawamgusi. Mfano nzuri ni mtumishi wa Mungu Ayubu, ambaye alikuwa huru pamoja na familia yake na kila kitu alichokuwa nacho. Shetani hakuweza kumgusa wala kumdhuru, kwa sababu alikuwa mkamilifu, na Mungu alimlinda kwa kumzingira. "Ayubu mtu huyo alikuwa mkamilifu na uelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepuka na uovu. Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema,.... Wewe hukumsingira kwa ukingo pande zote, pamoja na familia yake, na vitu vyote alivyo navyo? Ayu1:1,9." Kuishi maisha ya dhambi ni jambo baya sana. Kwa sababu Pepo wachafu wanaona wamepata nafasi na kuingia. "Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo.... Ndiyo itakavyo kuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.” Mathayo 12:45." Kuishi neno linavyosema unakuwa na mamlaka juu ya pepo wabaya.
Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa; "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka, Mathayo 11:12 ." " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu." Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...
Maoni
Chapisha Maoni