Neno mzaha lina maana ya utani. Mzaha au utani ni maneno ya uongo ambayo mtu husema yasiyo na maana ya kweli. Huku akifikiria Kufanya hivyo kwa lengo la kuwafurahisha wengine. Jambo lingine ambalo wanapaswa kulifahamu watoto wa Mungu ni kuepuka kufanya maigizo.
Ni muhimu kuwa makini na kutawala kinywa chako usinene maovu, maneno yasiyofaa, maneno ya hovyo ya mitaani (mzaha/masihara). Ikiwa mtu atasemezana na mtu mwingine kwa utani kwa kufanya hivyo atakuwa amesema uongo.
Neno la Mungu linafundisha mtu asifanye mzaha. Kwa sababu hiyo yatupasa maneno yasiyo maana tuyaepuke. Yesu alionya akasema,
"Basi, nawaambia, kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa. Mathayo 12:36-37 "Hukumu zimewekwa tayari kwa mwenye mzaha; Na mapigo kwa mgongo wa wapumba” (wanaofahamu). Mithali 19:2.
Hapa nitatoa mfano kuhusu mpumbavu. Ni yule mtu ambaye anayejua au kufahamu jambo lolote ambalo ni kinyume na neno Mungu na kulifanya kwa makusudi.
Zaburi 1 nayo inasema heri mtu yule asiyekaa vibarazani pa wenye mizaha.
JibuFutaDuh sawa
JibuFuta