KARAMA. Maana ya neno karama ni kipawa ambacho Yesu Kristo aliwapa Kanisa ambalo ni mwili wa Kristo wakati alipokuwa anapaa kwenda mbinguni. Sababu ya kutoa vipawa ilikuwa kama ifuatavyo:
1. Kanisa lijengwe na kukamilishwa.
2. Kazi ya huduma katika kanisa iweze kutendeka.
3. Kufikia umoja wa imani katika Kristo Yesu.
4. Kumfahamu sana Mwana wa Mungu.
5. Kuwa mtu mkamilifu kama Kristo.
6. Ili tusiwe kama watoto wachanga kwa kudanganywa na mafundisho ya uongo.
7. Kila kiungo kiweze kujengwa na mwenzake na kuwa na upendo.
Endelea kusoma kama ilivyoandikwa: "....Alipaa juu.... Akawapa wanadamu vipawa. Naye alitoa wengine kuwa; mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti; na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tuasiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. ....kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo." Waefeso 4:8,11-16.
Kutokana maandiko hayo ni muhimu kanisa liwe na vipawa. Kanisa likiwa na vipawa linaimarika akiroho na kusimama imara katika Mungu. Kanisa kama halina vipawa litakuwa vuguvugu na siku ya mwisho litakataliwa.

Maoni
Chapisha Maoni