"Bwana asema hivi, .... I wapi njia iliyo njema? mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsini zenu. ....” Yeremia 6:16. Njia njema ambayo Mungu amesema ni kuishi kwa kufanya neno lake linavyosema. Kwa sababu hiyo raha inapatikana kwa kumpendeza Mungu. Ndio maana mtumishi wa Mungu akasema, “Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.” Zaburi 40:8. “Ndio maana Yesu alisema, "Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;” Mathayo 11:29. Ili mtu aweze kuelewa maana ya neno raha nitaelezea kama ifuatao; Mtu mwenye raha anajisikia moyoni au nafsini mwake vizuri sana, kufarijika, utulivu, punziko na kuridika.
Pia wakati mtu mwenye dhambi anapomgeukia Mungu na kutubu anakuwa na raha moyoni ndio maana imeandikwa, “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;” Mitume 3:19. Maana ya neno kuburudishwa ni pale mtu anapofurahishwa moyoni au nafsini mwake.
Vilevile kuna raha ya mbinguni kwa wale wote watakaoingia. Imeandikwa, "Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wetu asije akaonekana ameikosa.” Waebrania 4:1.
Maoni
Chapisha Maoni