Kuna umuhimu wa mkristo aliyeokoka kutambua wema wa Mungu usiopimika. Ninasema hivyo kwa sababu Mungu aliupenda ulimwengu akamtoa mwana pekee Yesu Kristo aje duniani ili amwokoe mwanadamu kutoka katika dhambi. Mathayo 18:11,14 “[Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.] Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.” 2 Petro 3:9 “... maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba”. Kutokana na maandiko haya ni muhimu ukafahumu ya kwamba kwa wema wake Mungu amekupa nafasi ya kuusoma ujumbe huu ili utengeneze maisha yako kwa kutubu na kufanyika kiumbe kipya katika Mungu.
Jambo lingine ambalo unapaswa kulifahamu katika maisha yako ni kwamba umepewa nafasi moja tu. Nafasi hiyo ambayo umepewa ni wakati huu unaoishia hapa duniani. Hebu fikiria na kufahamu mwanadamu ni kama maua ambayo yapo katika matawi ya mti wakati wa asubuhi, lakini yakaanguka ghafla hata mcha haujafika. Petro 1:24 “Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. hukauka na ua lake huanguka;”
Ni muhimu kuwa makini na kuwa tayari wakati wote hujui saa wala siku ambayo utakufa au siku ambayo Yesu anarudi kulichukua kanisa lake. Ufunuo 3:3 "Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako."
Pia kuna andiko lingine ambalo linasema mwanadamu ni kama mvuke. Tukiangalia mvuke kwa kawaida huonekana kwa muda mfupi na baada ya hapo hupotea. Kwa hiyo vilevile mwadamu anaishi kwa muda mfupi hapa duniani. Kwa sababu hiyo si vema mtu kujisifu kwa ajili ya mambo ambayo atayafanya baadae. Hapa nitatoa mfano, kuna mtu mmoja ambaye bado hajaokoka halafu mtumishi wa Mungu akamjia muda wa saa tatu asubuhi na kumhubiria habari njema ya wokovu ili atutubu dhambi zake na kumpokea Yesu. Lakini mtu huyo akasema ngoja kwanza kuna shughuli ninafanya nitatubu saa tatu na nusu. Kichotokea kwa mtu huyo kabla ya saa tatu na nusu alikufa. Kwa sababu hiyo aliipoteza nafasi moja ambayo hawezi kuipata tena. Unaweza kuona mtu huyo alikuwa na nafasi moja ya muda mfupi.
Ndugu mkristo uliyeokoka ni muhimu kuutumia vizuri muda uliopewa wa kuishi hapa duniani mara moja tu. Mtu akifa katika dhambi hana nafasi ya kuwa hai tena na kurudi duniani ili atubu dhambi zake. Baada ya mwanadamu kufa anahukumiwa. Waebrania 9:27
“Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; Yakobo 4:13-14 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.”
“Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; Yakobo 4:13-14 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.”
Kuna sharti ambalo mtu mwenye dhambi anapaswa kulitimiza ili Mungu asamehewe anapotubu. Ni lazima awe ameweka nia ya kuachaa kufanya dhambi. Mithali 28:13 "Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye Aziungamaye na kuziacha atapata rehema". Lakini ikiwa mtu anatubu na bado anayo nia moyoni ya kuendelea kufanya dhambi hatasamehewa. Pia kuna jambo lingine kabla mtu hajatubu dhambi zake ni sharti asamehe watu waliomkosea, naye ndipo atasamehewa makosa yake. Mathayo 6:14-15
"Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu."
"Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu."
Mtu ambaye ametubu na kuacha kufanya dhambi, Mungu hatazikumbuka dhambi zake. Ezekieli 18:21-22 “Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi."
Vilevile ikiwa mtu ametubu dhambi zake hazitaonekana, wala hazitakuwapo kwa sababu zimefutwa. Kwa sababu hiyo mtu anakuwa na furaha kama andiko linavyosema katika kitabu cha Matendo 3:19 “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;”
Maoni
Chapisha Maoni