Nimeona ni muhimu kuelezea maneno mawili ambayo ni kuamini na kuokoka yanavyotumika katika Biblia. Maneno hayo tukiyaangalia tunaweza kuona yanatofautiana maana na matumizi yake. Haya maneno yanatumika kama ifuatavyo;
1.Neno kuamini maana yake ni kutumaini au kutarajia. Kutokana na maana ya maneno haya mtu anakuwa ni mwenye imani pale anapokuwa na uhakika wa yale mambo anayoyatumaini na kuyatarajia ambayo hayajaonekana au kutokea. “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” Waebrania11:1.
2.Neno kuokoka lina maana rahisi ambayo mtu yoyote anaweza kuelewa. Kwa mfano mtu mmoja amezama baharini lakini hawezi kuongealea na kujiokoa maisha yake asiangamie katika maji kwa sababu hana ujuzi wa kuogelea. Halafu akaja mtu mwenye nguvu na ujuzi wa akaogelea na kumwokoa kutoka katika maji. Kwa sababu hiyo, mtu huyo anakuwa ameokolewa au ameokoka kuangamia katika maji.
Kutokana na maana ya maneno haya hapa juu ambayo nimeyafafanua itakuwa ni rahisi wewe kuelewa kusudi la Mungu kuhusu kuokoka.
Kwa sababu mwanadamu ni mwenye dhambi Mungu alikusudia kumtuma Yesu Kristo kuja ulimwenguni ili awaokoe watu wote kutoka katika dhambi zao. Ndio maana imeandikwa; “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” Matendo ya Mitume 4:12.
Kutokana na maneno ya Mungu katika Biblia yanaonyesha wazi hakuna mwanadamu anayeweza kujiokoa mwenyewe kutoka katika dhambi zake na kuziacha. Ndio maana “Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.” Yohana 8:34-36. Hapa Yesu alikuwa akionyesha mtu anavyoitumikia dhambi kama mtumwa anavyomtumikia bwana wake aliyemwajiri wala hayuko huru. Iakini Yesu amedhihirisha wazi ya kwamba anao uwezo wa kumweka huru mtu mwenye dhambi.
amen
JibuFuta