Ruka hadi kwenye maudhui makuu

RAFIKI WA KWELI KATI YA MTU NA MWENZAKE.

Ili tuweze kufahamu maana ya rafiki wa kweli kati ya mtu na mwenzake, ni vizuri tukaangalia neno la Mungu linavyosema. Mungu wetu ndiye rafiki wa kweli kwa sababu yeye ndiye aliyetupenda kwanza. Tulipokuwa ni wenye dhambi, kwanza yeye alitupenda sisi watu ambao tulikuwa hatustahili mbele zake, kwa sababu yeye ni mtakatifu. Kwa upendo wake alimtoa na kumtuma mwanawe. Kupitia yeye sisi tulio na dhambi tuokolewe na kuishi katika upendo wa kweli wa Mungu. Kwa hiyo, inatupasa sisi kuishi katika urafiki wa kweli kati ya mtu na mwenzake. “Kwa maana jinsi Mungu alipenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee... hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye”. ( Yohana 3:16,17 ).

Jambo la muhimu.
Ni vizuri kufahamu ya kwamba marafiki wa aina mbili:

1.Rafiki wa kweli wakati wote.
Huyu ni rafiki anayependa kuwa na uhusiano wa karibu kati yako na wewe wakati wote. Wakati wa shida hakuachi wala kukuepuka. Huyu haangalii hali yako ya maisha kwamba wewe ni masikini au ni tajiri. Rafiki wa namna hii, huyo ndiye rafiki mwenye upendo wa kweli.

2.Rafiki ambaye siyo wa kweli.
Rafiki wa namna hii anapenda kuwa na uhusiano  na wewe kwa sababu ya vitu kama fedha, mali au cheo. Huonyesha kuwa na urafiki na wewe wakati ambao anahitaji kupata msaada au kitu chochote kutoka kwako. Lakini atakapofahumu ya kuwa huna anachokihitaji kama vile fedha, mali na cheo, bali ni mtu mwenye shida hawezi kuendelea kuwa na urafiki na wewe. Kwa sababu hiyo anakuacha na kukuepuka kabisa. Rafiki wa namna hii a maonyesho wazi ya kwamba hakuwa na upendo wa kweli kwa ajili yako. Bali alikuwa anapenda vitu alivyokuwa anatarajia kupata kwako

Fuatilia somo lingine kwa kubofya hapa upate kufahamu;  RAFIKI WA KWELI WA MUNGU

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa Roh

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu    - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi  kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea  Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi  maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa ajili ya kufanya uamuzi. Ndio maana Yesu  alipokuwa akifundisha  alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi kwa hiari maisha ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. “ "Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya,  kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana"   Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana  Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"     Walawi  19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawasawa na maagizo, sheria na taratibu . I