Ruka hadi kwenye maudhui makuu

RAFIKI WA KWELI WA MUNGU.

Karibu na endelea kujifunza neno la Mungu katika somo hili linalohusu rafiki wa kweli wa Mungu. Yampasa kila mkristo aliyeokoka kufahamu  ya kwamba yeye ni rafiki wa Mungu ikiwa anazingatia maagizo ya neno la Mungu  kama ifuatavyo;
1. Kumpenda Mungu na kudumu katika kuzishika amri zake.  “ Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nimtapenda na kujidhihirisha kwake”. (Yohana 14:21). “...Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuwa kwake, na kufanya makao kwake. Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; …” (Yohana 14:23,24).  

Kutokana na maandiko ya neno la Mungu  kama yanavyosema hapa juu, ni lazima  mtu awe na upendo wa kweli kwa Mungu kwa kuzishika  amri zake.  Ikiwa mtu hatazishika amri za Mungu huyo atakuwa  hampendi Mungu na wala si rafiki wa kweli wa Mungu. Kwa sababu hiyo mtu huyo hana upendo wa Mungu ukikaa ndani yake.

2. Kudumu katika upendo wa Mungu kwa kuzingatia kuishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema. “Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.” (Yohana 15:10-11). Katika maandiko haya yanaonyesha wazi ya kwamba mtu akikaa (akidumu) katika pendo la Mungu, mtu  huyo anakuwa na furaha ambayo Yesu anayo.

3. Kuwa na upendo kamili. Hili ni jambo la muhimu. Mtu  nayekuwa na upendo kamili ni mtu  ambaye anampenda Mungu na watu wengine. “...Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu”. (1Yohana  4:12). Mtu hawezi kusema anampenda  Mungu iwapo atakuwa  anamchukia ndugu yake. “Mtu akisema, nampenda  Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; Kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake”. (1Yohana 4:20-21).

4. Lazima mtu  amwamini Mungu na kuishi kwa imani. Tunaweza kujifunza kwa Ibrahim ambaye alikuwa ni rafiki wa Mungu kwa sababu alikuwa anamwamini na kufanya mambo  yote ambayo Mungu aliyomwagiza. “Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yake. Maandiko yale yakatimizwa yalivyonena, Ibrahim alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.” (Yakobo 2:22,23).

Kwa sababu hiyo unaweza kuona na kufahamu ya kwamba kuamini na kutenda ni vitu viwili tofauti. Kwanza Ibrahim alimwamini Mungu na pia alitenda sawasawa na Mungu alivyomwagiza. Imani ya namna hii, ndiyo imani iliyokamilika.  Haiwezekani mtu kumwamini Mungu peke yake bila kuyatenda aliyoagiza. Mtu afanyaye hivyo hawezi kuwa rafiki wa kweli wa Mungu. Ndio maana imeandikwa; “Mwaona ya kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake”. (Yakobo 2:24).

5. Kuishi kwa imani kwa kumwamini Mungu na kumtegemea katika mambo yote na kufahamu ya  kwamba yeye ndiye  msaada.  Kuishi kwa imani ya namna hiyo ndipo tunampedeza Mungu.

Ijapokuwa mtu atakuwa na mambo magumu au shida yoyote, yampasa kumtegemea na kumtumaini  Mungu kwa sababu yeye ndiye msaada katika maisha yetu. Ni muhimu kumtegemea Mungu na kumtumaini kwa sababu kuna mambo mengine kwetu sisi wanadamu hayawezekani, ila kwa Mungu yote yawezekana. Hapa tunaweza kuona anayemtegemea Mungu amebarikiwa na yule asiyemtegemea amelaaniwa. “Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, Na moyoni mwake amemwacha Mungu...Amebarikiwa mtu yule mtu anayemtegemea Bwana, ambaye Bwana ni tumaini letu”. (Yeremia 17:5,7). “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, Roho yangu haina furaha naye.” (Waebrania 10:38)

 Fuatilia somo lingine hapa kwa kubofya  upate kumfahamu, 




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa Roh

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu    - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi  kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea  Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi  maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa ajili ya kufanya uamuzi. Ndio maana Yesu  alipokuwa akifundisha  alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi kwa hiari maisha ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. “ "Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya,  kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana"   Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana  Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"     Walawi  19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawasawa na maagizo, sheria na taratibu . I