Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUFANYA YOTE KATIKA MAPENZI YA MUNGU.

Kwa  kusoma mafundisho ya somo hili
 utajengwa na kuimarishwa katika imani ya neno la Mungu. Kuna jambo la msingi ambalo ni la muhimu kwa kila mkristo aliyeokolewe. Yampasa kwa kila jambo analolifanya alifanye sawasawa na neno la Mungu linavyosema. Mojawapo ya mambo hayo ni ibada katika kuomba, kuabudu, kusifu na kucheza mbele za Mungu.

Matumizi yasiyo sahihi ya jina la Yesu.
Yatupasa kulitumia jina la Yesu kulingana na kanuni za neno laungu.
Hatuwezi kumtukuza na kumeshimu kama tunalitumia jina lake isivyo sahihi.
Namna isiyo sahihi ni hili ifuatayo;
Ikiwa mtu anatamka na kusema kwa Jina la Yesu ninavunja, ninaharibu na kukemea roho ya dhambi, laana, umaskini, magonjwa na mapepo. Hii siyo njia sahihi inayofaa kuondoa.

Njia iliyo sahihi na inayofaa ni kama ifuatavyo:
1. Kuondoa dhambi ni kwa njia ya kuweka nia na kuamua kuziacha na kutubu. "...Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema".  (Mithali 28:13). Ijapokuwa Mungu anamsamehe mtu dhambi pia huziondoa na wala hazikumbuki tena. Yeye Mungu anasema hivi; "Mimi, naam, mimi ndimi niyafutaye makosa yako  kwa ajili yangu mwenyewe; wala sitazi kumbuka dhambi zako." (Isaya 43:25).

2. Kuondoa laana ni wakati ambapo mtu anakuwa ameokolewa na kudumu kwa kuishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema, ndpo Kristo anakuwa amemweka huru mbali na laana kama andiko linavyosema; "Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanyika laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa , Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti." (Gal 3:13). 

3. Kuondoa umaskini ni wakati mtu anapokuwa na ubunifu na kufanya kazi kwa bidii. Na si hivyo tu yampasa mtu kuishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema. Naye Mungu humfanikisha katika kazi zake kama alivyosema, "Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kufanya maagizo yake yote leo, ... kwa kuibarikia kazi yote ya mkono wako.." (kumbukumbu 28:1, 12).

4. Kuondoa au kuepuka magonjwa kuna njia zifuatazo ambazo ni;
(a). Kudumu katika wokovu kwa kuishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema. Naye Mungu anasema; "Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema ayowaapia baba zako". "Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao" (Kumbukumbu 7:12, 15). kutokana hili andiko linavyosema linaonesha ya kwamba
 kuna magonjwa yanayotokana na dhambi, ambayo Mungu huyaweka au kuyaruhusu kwa wale watu watendao dhambi. Sasa yakupasa kuepuka dhambi. Lakini si kila mtu ikiwa anaumwa ametenda dhambi, bali inawezekana ikawa ni sababu nyingine.

(b). Kuepuka magonjwa kwa kula vyakula bora kama samaki, maziwa, mayai, karanga, mboga za majani, matunda, nyama, maharagwe na vyakula vya wanga kama mahindi, viazi na ndizi n.k.

(c). Njia nyingine ni kunywa maji mengi kiasi cha lita 3 kwa siku, ambapo yana faida nyingi katika mwili wa mwanadamu kama vile kuondoa uchafu na husaidia damu kusafiri. Maji yanasaidia akili ya mwanadamu kuwaza vyema zaidi, kuwa na kumbukumbu na husaidia mwili kuwa na  maji ya kutosha. Ikiwa mtu ni mnene na anao utaratibu wa  kunywa maji ipasavyo, hawezi kula chakula kingi. Kwa njia hii  hupunguza uzito, mwili huwa na  hewa ya kutosha katika misuli na kusababisha ngozi kuwa nyororo. Hizi ni baadhi faida nimezieleza lakini ziko nyingi zitokanazo na kunywa maji.  Kiwango cha maji ambacho nimekitaja
kimedhibitishwa na wataalamu wa afya.

(d). Kwa kuzingatia usafi wa mwili, chakula, maji, malazi na mazingira. Kunawa mikono kabla ya kula. Na pia Kunawa mikono baada ya kutoka chooni.

5. Njia ya kuwekwa huru mbali na  mapepo kwa mtu binafsi ni pale mtu anapokuwa ameokolewa na kudumu kwa kuishi sawasawa na neno la Mungu. Ikiwa mtu amepagawa na pepo, mtu wa Mungu aliye mtakatifu na mwenye mamlaka humwamuru amtoke. Naye humtoka mtu yule aliyempagawa na kuwa huru kabisa. Lakini ataendelea kuwa huru ikiwa atadumu katika utakatifu. Tunaweza kujifunza kupitia mtumishi wa Mungu Paulo alivyomtoa pepo kwa yule mtu aliyempagawa, alitamka kwa kusema  “..…nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo mtoke huyu, Akamtoka saa ile ile.” Mdo 16:18. Hii ndio njia sahihi ya kutoa  Pepo bila kupoteza muda. Ikiwa mtu wa Mungu hawezi kumtoa pepo kwa amri na mamlaka kwa wakati huo huo. Yampasa amtafute Mungu zaidi kwa maombi, kufunga na kudumu katika utakatifu. Baada ya kufanya hivyo atauona utukufu wa Mungu na malamka yake.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...