1. Matumizi ya vyombo vya muziki wakati wa kusifu, kuabudu na kuimba mbele za Mungu katika ibada inapasa maneno ya wimbo yasikike vizuri. Hili linawezekana iwapo sauti ya upigaji wa vyombo itakuwa ya wastani. Kama sauti ya vyombo ikiwa juu sana inameza usikivu wa maneno ya wimbo. Kwa sababu hiyo maneno ya wimbo hayasikiki ipasavyo na inakuwa ni makelele katika ibada. Haya nimeyaeleza kwa ajili ya kuelimisha, kwa sababu katika sehemu mbalimbali za ibada nimeona na kushuhudia maneno ya wimbo hayasikiki ipasavyo kutokana na sauti ya vyombo kuwa juu kuliko sauti ya maneno ya wimbo.
Jambo lingine la muhimu kwa waimbaji katika ibada wanalopaswa kulizingatia ni kujifunza na kuwa stadi katika kusifu na kuabudu. Kuna andiko linadhibitisha na kusema; "Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia Bwana, wote walikuwa wastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane" Nyakati 25:7.
2. Matumizi ya kipaza sauti ( mikrofoni) haipaswi kuwekwa karibu sana na mdomo. Ikiwa kitawekwa karibu sana na mdomo sauti haitasikika vizuri bali itakuwa sauti ya makelele na kuwakera wasikilizaji. Jambo lingine la muhimu kuzingatia kuhusu kipaza sauti ni kuhakikisha kinatoa sauti iliyo sawasawa ili kusikika vizuri. Kwa kufanya hivyo usikivu wa sauti unasikika vizuri na kuwavutia wasikilizaji.

Maoni
Chapisha Maoni