Maana ya neno wokovu na linavyohusiana
Mwanamke alipoona yakuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, na ni mti watamanika kwa maarifa, basi alitoa matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala. "Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako, michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za bondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi” Mwanzo 3:6,17-19. Kama ambavyo umesoma haya maandiko hapa juu, matunda waliyokula, ni kama maembe, mapapai, machungwa na kadhalika.
Adamu na Hawa kuondolewa Edeni. Kama hawakula hayo matunda amri ya kifo isingetenda kazi bali wanadamu wangeishi milele, ndio maana akawafukuza watoke katika bustani ya Edeni kwa sababu watakula matunda ya uzima na kuishi milele.“Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatoa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi (Malaika), upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko,kuilinda njia ya mti wa uzima” Mwanzo 3:22-24.
Wanadamu wote ni wenye dhambi na kifo kimewafikia.
Kutokana na uthibitisho wa maandiko ya neno la Mungu ambayo nimeyaandika yanaonyesha mwanadamu hastahili mbele za Mungu bila kuokolewa na Yesu. Hakuna mtu yeyote awezaye kujiokoa mwenyewe kutoka katika dhambi bila kupitia jina la Yesu. "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” Matendo 4:12. kuokoka ni jambo la msingi na thamani kuu kupita yote ya ulimwengu huu ambao sisi ni wasafiri na wapitaji. Hakuna anayeishi milele hapa duniani.
Mtu anapokufa anahukumiwa wakati huo huo.
“Ikawa yule masikini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu.Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, unihurumie, umtume Lazaro achomvye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu” Luka 16:22-24." andiko lingine linasema; ”Kama vile watu walivyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” Waebrania 9:27. Kutokana na Andiko hili linaonyesha wazi mwanadamu amepewa nafasi moja tu kuishi hapa duniani. Kwa sababu hiyo yampasa mtu kuwa makini na akizingatia kuishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema, na kudumu katika utakatifu. Ni muhimu kila mtu kuwa tayari ili inapotokea Yesu akarudi ghafla au mtu anapokufa awe na haki ya kuingia mbinguni. Ni jambo la muhimu kufahamu ya kwamba kifo humtokea mtu kwa wakati wowote. Je! Wewe uko tayari kwa ajili ya ufalme wa Mungu? kama bado fanya uamuzi sasa. Usikubali kupoteze nafasi ambayo umepewa na Mungu. Kumbuka umepewa nafasi mara moja tu.
Ni muhimu kuokoka, kubali sasa.
Asiyekubali kuokoka atahukumiwa. Anayekubali kuokolewa atakuwa na uzima wa milele,
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe pekee,ili kila mtu amwamiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiye mwamini amekwisha hukumiwa;kwa sababu hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu. Amwaminiye mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini mwana hataona uzima, bali ghadabu ya Mungu inamkalia” Yohana 3:16 -18, 36.
Jinsi ya kuokoka.
Ni muhimu utambue yakuwa wewe ni mwenye dhambi na kuamua kugeuka na kumfuata Yesu. Kwa kuungama na kuziacha dhambi. Yesu, “Akasema amin, nawaambia, Msipoongoka (kugeuka) na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” Mathayo 18:3. “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema” Mithali 28:13. "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudshwa kwa kuwako Bwana". Matendo 3:19.
Sala ya kuokoka
Baada ya kusema sala hii umempokea Yesu yuko pamoja nawe. Ungana na kanisa la watu anbao wameokoka ukajengwe kiroho katika neno la Mungu kwa ukamilifu wake. Na siku ile tuonane mbinguni.
Kinachotokea unapookoka:
3. Unafanyika upya na kuanza maisha mapya. “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! yamekuwa mapya” 2Wakorintho 5:17.
4. Unafanyika mtoto wa Mungu. “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”. Yohana 1:12.
Neno wokovu lina maana ya kuokoa, kwa mfano meli ya abiria imepata hitilafu inaanza kuzama katika maji wanakuja watu kuwaokoa waliomo ndani ya meli kabla haijazama ndani ya maji na watu kuangamia. Watu ambao wameokolewa wameokoka kuangamia katika maji. Mungu alimtuma Yesu Kristo aje duniani awaokoe wanadamu kutoka katika dhambi wasiangamie na kuhukumiwa kwenda jehanum ya moto na kuteseka milele. Ndio maana malaika wa Bwana alitumwa na Mungu akamwambie Yusufu Mume wa Mariamu yakwamba mkewe ana mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, atamzaa mwana atamwita jina lake Yesu. Maana ya jina Yesu ni Mmokozi. Kwa hiyo alikuja kuwaokoa watu kutoka katika dhambi “Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu Mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu; kabla hawajakaribiana alionekana ana mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu....Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewakoa watu wake na dhambi zao”. Matayo 1: 18-21.
Ni jambo la muhimu sana ulimwengu kutambua yakwamba Yesu aliacha enzi na mamlaka mbinguni akaja duniani kwa ajili ya ulimwengu ili uokolewe katika yeye. Neno "ulimwengu" linamaanisha yakwamba ni wanadamu waishio katika dunia hii. Kwa sababu hiyo Mungu alikusudia awaokoe watu wote. Ndio maana imeandikwa, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele". Yohana 3:16.
Dhambi, kifo na laana ilivyotokea.
Mwanadamu yeyote katika vizazi vyote ni muovu na mwenye dhambi, kutokana na asili ya dhambi kwa wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa kutokana na matunda waliokula ambayo Mungu aliwaagiza wasile ndio maana hakuna mwenye haki hata mmoja wote wamepotoka.“Bwana Mungu akamwagiza huyu mtu, akisema, matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika” Mwanzo 2:17.
Mwanamke alipoona yakuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, na ni mti watamanika kwa maarifa, basi alitoa matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala. "Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako, michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za bondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi” Mwanzo 3:6,17-19. Kama ambavyo umesoma haya maandiko hapa juu, matunda waliyokula, ni kama maembe, mapapai, machungwa na kadhalika.
Adamu na Hawa kuondolewa Edeni. Kama hawakula hayo matunda amri ya kifo isingetenda kazi bali wanadamu wangeishi milele, ndio maana akawafukuza watoke katika bustani ya Edeni kwa sababu watakula matunda ya uzima na kuishi milele.“Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatoa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi (Malaika), upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko,kuilinda njia ya mti wa uzima” Mwanzo 3:22-24.
Wanadamu wote ni wenye dhambi na kifo kimewafikia.
Hakuna mwenye haki hata mmoja kwa sababu wanadamu ni uzao wa Adamu.“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni,na kwa dhambi hiyo mauti; na hiyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”. Warumi 5:12. “Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la hata mmoja” Warumi 3:10 -12.
Kutokana na uthibitisho wa maandiko ya neno la Mungu ambayo nimeyaandika yanaonyesha mwanadamu hastahili mbele za Mungu bila kuokolewa na Yesu. Hakuna mtu yeyote awezaye kujiokoa mwenyewe kutoka katika dhambi bila kupitia jina la Yesu. "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” Matendo 4:12. kuokoka ni jambo la msingi na thamani kuu kupita yote ya ulimwengu huu ambao sisi ni wasafiri na wapitaji. Hakuna anayeishi milele hapa duniani.
Mtu anapokufa anahukumiwa wakati huo huo.
Imeandikwa mtu baada ya kufa anahukumiwa wakati huo huo ikiwa amekufa katika dhambi au utakatifu. Kulikuwapo na masikini aliyeishi maisha ya utakatifu na tajiri aliyeishi maisha ya dhambi. Kila mmoja alipewa hukumu yake. Yule masikini aliwekwa mahali salama peponi. Yule tajiri aliwekwa kuzimu mahali pa mateso ya moto.
“Ikawa yule masikini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu.Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, unihurumie, umtume Lazaro achomvye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu” Luka 16:22-24." andiko lingine linasema; ”Kama vile watu walivyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” Waebrania 9:27. Kutokana na Andiko hili linaonyesha wazi mwanadamu amepewa nafasi moja tu kuishi hapa duniani. Kwa sababu hiyo yampasa mtu kuwa makini na akizingatia kuishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema, na kudumu katika utakatifu. Ni muhimu kila mtu kuwa tayari ili inapotokea Yesu akarudi ghafla au mtu anapokufa awe na haki ya kuingia mbinguni. Ni jambo la muhimu kufahamu ya kwamba kifo humtokea mtu kwa wakati wowote. Je! Wewe uko tayari kwa ajili ya ufalme wa Mungu? kama bado fanya uamuzi sasa. Usikubali kupoteze nafasi ambayo umepewa na Mungu. Kumbuka umepewa nafasi mara moja tu.
Ni muhimu kuokoka, kubali sasa.
Mtu ni lazima azaliwe mara ya pili (kuokoka) na kufanyika kiumbe kipya, ndipo atauona ufalme wa Mungu na kuingia. “Yesu akajibu, amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu” Yohana 3:3,5. “Wakati wa wokovu ni sasa, kwa maana asema, wakati uliokubalika nalikusikia, siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama siku ya wokovu ndio sasa”.
2Wakorintho 6:2.
Asiyekubali kuokoka atahukumiwa. Anayekubali kuokolewa atakuwa na uzima wa milele,
Kufa kwa mwadamu ni wakati wowote.
Kama hujaokoka bado ungali mwenye dhambi jiulize swali kama ukifa sasa utakwenda wapi? Ukisema utaokoka wakati mwingine unajuaje utafikia huo wakati ungali hai?. Endelea kufikiria kwa makini ni wangapi walikufa ghafla bila kujua wala kutarajia?. Kwa mfano mtu anasema moyoni mwake siokoki leo nitaookoka kesho kumbe roho yake inachukuliwa leo na kuhukumiwa kwenda jehanaum ya moto na kuteseka. Mwili wa mwanadamu ni kama majani na maua. Kwa sababu leo upo kesho haupo. Ndio maana imeandikwa hivi,“Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na jani lake huanguka” 1Petro 1:24.
Jinsi ya kuokoka.
Sala ya kuokoka
Wewe ambaye unakubali kumwamini na kumpokea Yesu Kristo akuookoe na dhambi zako.Fuatisha sala hii kwa kusema; Ee Mungu Baba ninatabua, mimi ni mwenye dhambi, unihurumie na kunisamehe, uniweke huru na safi, kwa damu ya mwanao Yesu Kristo, iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu. Kuanzia sasa ninaamua kukugeukia kabisa na kumpokea Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yangu.Ninakuomba na ninakushukuru kwa jina la Yesu Kristo. Amen.
Baada ya kusema sala hii umempokea Yesu yuko pamoja nawe. Ungana na kanisa la watu anbao wameokoka ukajengwe kiroho katika neno la Mungu kwa ukamilifu wake. Na siku ile tuonane mbinguni.
Kinachotokea unapookoka:
1. Yesu anaingia ndani yako. "Tazama, nasimama mlangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami”. Ufunuo 3:20.
2. Unapata haki na wokovu. “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki,na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” Warumi 10:10.
3. Unafanyika upya na kuanza maisha mapya. “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! yamekuwa mapya” 2Wakorintho 5:17.
4. Unafanyika mtoto wa Mungu. “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”. Yohana 1:12.
5. Unakuwa na uzima wa milele. “Na huu ndio ushuhuda,ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika mwanawe.Yeye aliye naye mwana, anao huo uzima; asiye naye mwana hana huo uzima". 1Yoh 5:11-12l
Maoni
Chapisha Maoni