Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ALIYEOKOKA KUTHIBITISHA UTAKATIFU.

Mkristo aliyeokoka ni muhimu kuthibitisha kama yeye ni mtakatifu. Kwa sababu Sifa ya Mungu yeye ni Mtakatifu, naye anataka tuwe watakatifu kama yeye alivyo. Ndio maana Mungu amesema; "...Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu."(Law 19:2). Yampasa mtu kuchunguza moyoni mwake ili aweze kufahamu ya kwamba je! Yeye ni mtakatifu? Jinsi ya kuthibitisha na kuwa na uhakika ni kama ifuatavyo;

1. Anaishi sawasawa neno la Mungu linavyosema. Hatawaliwi na dhambi katika maisha yake, kwa sababu emeweka nia moyoni mwake kutenda yaliyo ya haki. kwa sababu hiyo dhambi haina nguvu wala haiwezi kumtawala katika maisha yake kwa kuwa amekufa katika mambo ya dhambi. Ndipo katika maisha yake andiko hili lifuatalo litatimia kwake; "Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi... lakini kwa kule kuishi kwake, amwishi Mungu. Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu."  (Rum 6:10-11). "Yeye mwenyewe alizichukua dhaambi zetu katika mwili wake juu ya mti, ili, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki..." (1Pet  (2:24).

2.
Moyoni anayo amani na utulivu kwa kuwa hakutenda dhambi, wala hana hila ndani yake. Kwa sababu hiyo hakuna hukumu katika moyo wake. "Wapemzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu." (1Yoh 3:20-21). Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila. (Zab 32:2).

3. Anatunza utakatifu katika maisha yake. Ni pale mtu anapoweka nia moyoni hatatenda dhambi na kudumu kwa kutenda sawasawa na neno la Mungu linavyosema. Na ndio maana imeandikwa; "Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi." (1Yoh 5:18). 

4. Anakuwa na amani moyoni na watu wote. Hili ni jambo la muhimu katika maisha ya mkristo aliyeokoka kuwa na amani na watu wote. Ikiwa mtu hana amani na watu wote hatakuwa na utakatifu. "Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu akayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo."  (Ebr 12:14, 15).

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...