Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUWA NA UMOJA NA MUNGU.

Karibu katika somo mbalo linakuhusu wewe kuwa na umoja na Mungu na Yesu Kristo. Umoja ninaofundisha katika somo hili ni ule unaotokana na mtu aliyemwamini Yesu na kuokolewa, na kuamua kuishi sawasawa na maneno ya Mungu  yasemavyo. Mtu kama huyo anakuwa ni mtakatifu kama Mungu alivyo mtakatifu. Ndio  maana Yesu akasema. "Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake." (Yoh 14:23). "Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli  kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake." (1Yoh 2:5)

Wale walio watakatifu ndio ambao Mungu amewapa haki ya kuwa na umoja na yeye. Ndio maana imeandikwa, "Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu..." (Yoh 15:3-4). Tunaweza kuona Bwana wetu Yesu Kristo alivyomwomba  Mungu kwa ajili yao watakaomwamini ili wawe na umoja na yeye na Baba. "Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu usadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma."  (Yoh 17:20-21).

Kuna  umuhimu ambao ni jambo la msingi, Mwamini kukamilishwa katika umoja na Mungu. Anakamilishwa kwa kuishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema, na pia Baba na Mwana wanapofanya makao ndani yake. Ndio maana Yesu akasema alipokuwa akiomba, "Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi." (Yoh  17:23). 

Vilevile tunapaswa kuwa na umoja sisi kwa sisi ambao Yesu alipokuwa akiomba mbele za Mungu alisema hivi; "Nami utukufu ule nimewapa wao; ili wao wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja." (Yoh 17:22 ). Huo ndio umoja wa kweli ambao Mungu alikusudia tuwe nao. Kwa sababu hiyo tunaweza kuona ni mpango wa Mungu kuweka kanuni ili wale wote wanaomtii katika neno  lake waishi katika umoja, kati yao na yeye.

Kuwa na umoja na Mungu kuna faida zaidi ya tunavyoweza kufahamu, lakini  Yesu ametuahidi ya kuwa aliye umoja naye akiombacho chochote atafanyiwa. "Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa" (Yoh 15:7).  

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...