Hapa tutaangalia mtu ambaye anaweza kuwa na uwezo wa kuomba na kuabudu katika Roho Mtakatifu ni Mkristo ambaye ameokoka na kumtii Mungu kwa kuishi sawasawa na neno lake. Na ndipo anajazwa Roho Mtakatifu, naye Roho atajidhihirisha kwake kama ifuayavyo;
1. Atasikia au kuhisi nguvu ndani yake anapokuja Roho Mtakatifu juu yake. Tunaweza kuona kwa uthibitisho wa maandiko haya yafuatayo, "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu..." Matendo 1:8. Katika andiko tunaweza kuona mtumishi wa Mungu Daudi alipotiwa mafuta na nabii Samweli kuwa Mfalme wa Israel. Roho Mtakatifu alikuja juu yake kwa nguvu. "Ndipo Samweli akaitoa pembe yake ya mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya Bwana ikamjia Daudi kwa nguvu tangu siku ile." 1Samweli16:13.
2. Ataongozwa na Roho Mtakatifu kunena kwa lugha mpya ambayo hajawahi kuisikia wala kufundishwa. "Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka." Matendo 2:4.
Ni jambo la muhimu na inatupasa kuomba katika uwepo wa Roho Mtakatifu. Na ndiyo maana Mitume walifundisha na kuonyesha umuhimu wa kuomba katika Roho. "Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho..." Waefeso 6:18. "Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu." Yuda 1:20.
Pia ni dhahiri kutokana hili fundisho hapa juu, vilevile ni jambo la muhimu kumsifu na kumwimbia Bwana katika Roho Mtakatifu. Na si hivyo tu, pia unaweza kumshukuru Mungu katika Roho Mtakatifu. Yesu alipowatuma wale wanafunzi wake kuihubiri habari njema waliporudi wakampa taarifa ya kwamba waliwatoa pepo juu ya watu waliokuwa wamepagawa nao walitii. Ndipo Yesu alimshukuru Mungu katika Roho Mtskatifu. "Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili, umewafunulia waatoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza." Luka 10:21.
Ninayo furaha kuu ndani yangu kwa kuwa ninaye Roho Mtakatifu, naye hububujika kutoka ndani yangu kama maji yanayobubujika katika chemichemi isiyokoma. Na ashukuriwe Mungu wa utukufu wote milele na milele. Amina. Ikiwa umemwishia Mungu kwa kujitolea kwake kama sadaka iliyoteketezwa madhabahuni pa Mungu, ndipo utauona utukufu wa Mungu ukishuka juu yako kwa nguvu na Roho Mtakatifu akibubujika kutoka ndani yako. Haleluya! Ni jambo la kufurahisha sana. Ndio maana imeandikwa; "...Yesu akasimama akapasa sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe, aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye..." Yohana 7:37-39.
Wakati ambao mtu anaweza kububujika katika Roho ni kama ifuatavyo; Ni pale mkirsto anapoabudu, kusifu, kuimba. Na Kuomba. Lakini kububujika kwa Roho hutokea ndani ya mtu ikiwa anazingatia kanuni aliyoiweka Mungu ambayo Yesu aliifundisha akisema; " saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo wamwabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa
Kumwabudu katika roho na kweli" Yohana 4:23-24.
Hapa nitaelezea jinsi mtu anavyomwabudu Mungu kwa roho na kweli ni kama ifuatavyo. Ni pale mtu anapodumu kwa kuishi sawasawa na neno la Mungu lisemavyo. Maana ya neno kweli ni neno la Mungu.
Ibada yetu ili ikubalike kwa Mungu na kumpendeza yatupasa kuitoa miili yetu kuwa viungo vya haki kwa Mungu.
"...Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msifuatishe namna ya dumia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapeni ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu." Warumi 12:1-2. " Basi dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa Zake; wala msiendelee kuvitoa viungo veynu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki." Warumi 6:13.
Maoni
Chapisha Maoni