Jambo la kwanza ninamshukuru Mungu kwa neema yake aliyonipa kufundisha neno lake. Ndungu mpendwa ninajua ya kwamba Mungu alikupenda sana, hata akamtoa Mwana wake wa pekee Yesu Kristo kwa ajili yako ili akukomboe kutoka katika dhambi zote ikiwemo dhambi ya uzinzi na uasherati. Sasa ninakusihi kwa neema ya Mungu fuatana nami kwa makini kuhusu somo hili nawe utauna utukufu wa Mungu katika maisha yako.
Tunaweza kuangalia kwa makini dhambi ya uzinzi na uasharati ambayo mtu akiitenda inaharibu ufahamu wake na hatimaye kuangamia. Mtu anapoteza uhusiano wake na Mungu, mawasiliano kati yake na Mungu yanakatika. Mungu ni Makatifu hana ushirika na wenye dhambi. “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” Mithali 6:26. “Lakini maovu yenu yamewafarikisha (yamewatenganisha) ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” Isahau 59:2.
Atendaye dhambi ya zinaa au uasherati kamwe hawezi kupata utoshelevu (kuridhika au kutosheka) kwa sababu tendo hilo ni kinyume na sheria ya Mungu na limelaaniwa. Ndiyo maana imeandikwa; “...wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.” Wagalatia 5:16. Mtu akishanaswa katika dhambi hiyo asipotubu hawezi kuwa huru katika maisha yake, bali atakuwa anateseka kwa kutumikishwa katika dhambi hiyo. Bali mtu akiwekwa huru anakuwa na amani na furaha.
Ndugu mpedwa ninaamini ya kwamba kutokana na andiko hili hapa juu linaonyesha wazi ya kwamba mtu hawezi kupata utoshelevu katika zinaa. Kwa sababu hiyo mtu anaweza kupata utoshelevu kwa mkewe au kwa mumewe wa halali.
Kwa wale waliokoka au kuzaliwa mara ya pili.
Wakati mtu alipookoka alimaanisha kutubu dhambi zake zote na kuziacha, ndipo Mungu alimsamehe sawasawa na ilivyoandikwa; “...Aziungamaye dhambi zake na kuziacha atapata rehema (atasamehewa).” Mithali 28:13. Kwa yule ambaye amekwisha okoka amewekwa huru mbali na dhambi, hatumikii dhambi. “...Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.” Yohanan 8:34,36. “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! Yamekuwa mapya.” 2Wakorintho 5:17.Hawezi kutenda dhambi ikiwa atazingatia kuishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema.
Jambo ambalo yakupasa kufanya ni kujilinda na kuepuka vishawishi ambavyo vinaweza kukusababishia utende dhambi. Pia unapaswa kuwa na kiasi pamoja na kujiwekea mipaka kwa mtu ambaye siyo mkeo au mume katika mahusiano. Mahusiano ninayosema ni yale ambayo yanaweza kuwa ya kikazi kama biashara, kilimo, kazi za ofisini, masomo na nyinginezo. Mkristo aliyeokoka na kusimama imara katika neno la Mungu hatakuwa na tamaa ya mwili kwa sababu amekwisha sulubishwa na Kristo ili asitende dhambi. “Tukijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena.” Warumi 6:6. Mstari huu unaonya au kukataza mtu aliyekwishaokoka asitende tena dhambi. Kwa hiyo ni muhimu kuzingatia maarifa ya neno la Mungu ambalo litakuongoza. Neno litakusaidi kujua jinsi ya kuishi kwa utaratibu ili usije ukavutwa na tamaa za kila namna, mojawapo ikiwemo tamaa ya mwili.
Dhambi inavyoanza ndani ya mtu.
Dhambi yoyote huanza ndani ya moyo wa mtu anapoanza kuwaza mawazo mabaya katika moyo wake. Ni vyema kutambua kuwa unapowaza mawazo mabaya unakuwa umetenda dhambi. Ikiwa mtu akimwona mtu asiyekuwa mkewe au mumewe na akamtamani moyoni mwake, huyo amekwisha kuzini. Ndiyo maana Yesu alifundisha akisema; “Mmesikia kwamba imenenwa, usizini; Lakini mimi nawaambia, mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Mathayo 25:27-28.
Mambo ambayo unapaswa kuzingatia ili uweze kushinda dhambi.
Sehemu hii nitafundisha jinsi ya kushinda na kuishi katika furaha ya wokovu. Yafuatayo ni mambo ya kuepuka ambayo yana ushawishi kwa mwanaume na mwanamke:
1. Kutokuangalia picha kwenye mtandao ambazo zinaonyesha wanaume na wanawake wakikutana kimwili. Vilevile kuepuka kusoma magazeti au vitabu vyenye mambo machafu yanayohusiana na zinaa.
2. Kutokufanya mizaha kati ya mwanaume na mwanamke. Hapa nitatoa kisa ambacho nilikiona siku moja. Siku hiyo nilimwona mwanaume mmoja akimwambia mke wa mtu mwingine unapendeza. Kufanya hivyo ni jambo baya kwa sababu huyo si mke wake. Kisa hiki kinaonyesha kwa uhalisi ni mojawapo ya mzaha. Kila mtu ana uhalali mbele za Mungu ikiwa anavutiwa na mkewe au mumewe na kumwambia unapendeza au ninakupenda. Hata hivyo kitendo hiki kinatakiwa kifanyike pale ambapo wako peke yao na haya ndio maadili. Yakupasa ujue mambo yanayofaa kumwambia au kumfanyia mkeo au mumeo mnapokuwa mbele za watu.
3. Kuulinda moyo wako ili usiyaruhusu mawazo mabaya kuingia. Ni muhimu kutambua ya kuwa dhambi yoyote inaanzia moyoni kwa kuwaza. Yakupasa kuamua kuutawala moyo wako na kutambua lipi linafaa kuwaza na lipi halifai na kuliacha. Haiwezekani usilolitaka kuwaza likapata nafasi na kukaa katika moyo wako. Wewe mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kuruhusu wazo lolote liwe jema au baya. Ndiyo maana imeandikwa; “Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya... Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.” Mathayo 12:33, 35. Utakapoulinda moyo wako usiwaze mabaya unaweza kuutawala mwili. “Kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili (kuutawala mwili) wake katika utakatifu na heshi huu n jihadharima. Si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.” 1Wthesalonike 4:4-5, 7.
Kama ulianguka katika dhambi.
Baada ya wewe kulisoma somo hili sasa ni wakati ambao Mungu amekujalia ili uweze kumgeukia. Yeye ni mwaminifu atakusamehe na kukuweka huru kutoka katika dhambi. Yafuatayo ni mambo yakupasayo kufanya:
1. Weka nia moyoni na kuamua kuacha kufanya dhambi.
2. Ungama mbele za Mungu kwa kukiri makosa uliyoyafanya na yale yaliyofichika ili akusamehe.
3. Weka nia mbele za Mungu ya kwamba kuanzia sasa hutaki kufanya tena dhambi, bali utadumu katika sheria zake.
4. Mshukuru Mungu kwa wema wake amekusamehe, na pia kwa sababu alikujalia kuwa hai kwa uvumilivu wake hadi leo hata ukatubu. Kuna wengine wamekufa katika dhambi bila kuzitubia, lakini wewe haukuwa mwema kuliko wao.
5. Omba kila siku na wakati mwingine funga ili uweze kusimama imara katika neno la Mungu. “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; lakini roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.” Mathayo 26:41. Andiko hili linadhihirisha wazi ya kwamba mtu akikesha (akidumu) katika kuomba hawezi kutenda dhambi. Ndiyo maana andiko hili linaonyesha kuwa kuna kujaribiwa lakini yule mtu ambaye anaomba hataingi katika majaribu. lakini kwa mtu yule ambaye haombi akijaribiwa na yule mwovu ni rahisi kutenda dhambi.
6. Vunja uhusiano na yule mwanamke au mwanaume uliyeanguka naye katika dhambi ya uzinzi.
7. Vunja mazoea yaliyopitiliza ambayo si ya kawaida uliyokuwa nayo kwa mtu ambaye si mkeo au mumeo.
8. Jihadhari na kuepuka wale wote ambao unajua wanaweza kukushawishi ili ufanye nao dhambi ya uzinzi.
Kwa kuzingatia hatua hizo unageuzwa na kuwa mtu mpya katika utakatifu. Nawe utauona uzuri wa Mungu ulivyo mkuu ndani yako kuliko mambo ya mwili. Kwa neema ya Mungu na Yesu Kristo hakika utazidi kuuona utukufu wa Mungu, ukuu wake, nguvu zake na wema wake usiopimika kwa mwanadamu.
Usipozingatia kanuni ambazo nimefundisha utashindwa na kuanguka katika dhambi mara kwa mara. Udanganyifu wa shetani utaingia ndani ya moyo wako ya kwamba haiwezekani kuishi bila kufanya dhambi. Kwa wale ambao wamezingatia sheria na kanuni ya neno la Mungu dhambi haina nafasi ndani yao. Wamewekwa huru hawatawaliwi tena na dhambi.
Sasa ninamwomba Mungu Baba kwa ajili yako ikiwa umenaswa kwenye dhambi yoyote, Mungu akujalie uwezo wa kushinda na kudumu katika mapenzi yake. Ni kwa jina la Yesu
Kristo ninaomba na
kumshukuru Mungu, Amen.
Asante kwa Neno zuri. Mungu akubariki
JibuFutaAhsante sana mtumishi wa Mungu.
JibuFutaMungu akubariki sana nimepata vitu vya kunitoa sehemu moja nakunipeleka sehemu nyingine
JibuFutaNeno zuri sana, ubarikiwe mtumishi wa bwana.
JibuFutanimesoma mwaka 2018 lakini ujumbe huu umekua baraka sana!! maana umenijenga sana. namshukuru Mungu nimepata kitu. Mungu akubariki sana.
JibuFutaAsante Mungu akubariki
JibuFutaAsante sana Mtu wa Mungu, tuzidi kuombeana maana hii dhambi ya uzinzi imekisiri sana upande wangu.
JibuFutamtumishi wa mungu ubarikiwe sana kiukweli nimekuwa nikitenda dhambi hii kwa takribani miaka yote niliyo nayo tangia kujifahamu nakingine zaidi huwa naumia sana ninapomaliza kufanya tendo kwa ninafahamu fikra kwamba nimemkosea mungu wangu daah mtumishi yani umenigusa mimi moja kwa moja .
JibuFutaUbarikiwe sana munishi wa MUNGU
JibuFutaSomo zuri sana na Mungu anisaidie niwe huru kweli kweli, Amen
JibuFutaBwana akubariki.
JibuFutaAsante mtumishi wa MUNGU nayapokea mafundisho yako kwa jina la yesu kristo bwana wangu AMINA
JibuFutaUjumbe umenigusa sana,naomba Mungu anisaidie sana.
JibuFutaMungu akubariki sana sana nimepata kitu hapa
JibuFutaAsante Sana mtumishi wa MUNGU, nimeguswa na SOMO hili moja kwa moja, Mungu anisaidie niweze kuyashika mafundisho haya
JibuFutaAmen SoMo nzuri
JibuFutaAmina napata nguvu
JibuFutaUbarikiwe mtumishi wa Mungu
JibuFutaNimebarikiwa sana mtumishi
JibuFutamungu aendelee kukujaza roho mtakatifu katika kufanya kazi yake na kuokoa roho za watoto wa mungu amina.
JibuFutaI blessed with article. God bless you and keep going
JibuFutaAmina mtumishi wa Mungu. Ubarikiwe kbs uzidishiwe tumefundishika kbs
JibuFutaAsante sanaa
JibuFutaNimeguswa sana na somo hili. Ninakiri nimekuwa natenda dhambi hii baada ya kusalitiwa na mwenzangu wa ndoa. Tukio lile lilinivunja moyo na kuona sina thamani ndipo nikaanguka na sikuweza kujinasua. Namshukuru Mungu kwa somo kwani baada ya kutenda nilipoteza tumaini la kusamehewa na Mungu lakn kwa somo hili limenipa tumaini mpya. Nimetambua kuwa sikuwa imara na hasira ya kusalitiwa ilinipeleka kwenye dhambi ileile niliyoichukia ilipotendwa na mwenzangu... Mungu namwomba anisamehe na ninataka kusimama tena bila kujali matendo au moni ya wengine. Uendelee kutupa maarifa haya ya rohoni.
JibuFutaAsante sana mtumishi
JibuFuta