Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TUNDA LA UVUMILIVU.

Hili ni tunda ambalo linaonyesha uvumilivu wa Mungu kwa wanadamu, ijapokuwa ni wenye dhambi, amewavumilia na kuwapa muda wa kumgeukia na kutubu. Yeye Mungu si mwepesi wa hasira anawahurumia watu wake na kuwavuta kwa upendo wake ili watubu. “....Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe....” Kut 34:6,7.

Tunaendelea kujifunza kuhusu uvumilivu wa Mungu, kabla hajaleta ngarika ya maji duniani na kuwaangamiza wanadamu kwa sababu ya maovu waliyokuwa wanayatenda, aliwapa muda kama wangetubu. “Watu wasitii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa kitengenezwa; ambao ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka katika maji.” 1Pet 3:20. Wengine wote ambao hawakutubu waliangamizwa kwa ngarika ya maji, kama andiko linavyosema, “Kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu.” Rum 9:22.

Kutokana na maandiko hayo tunaweza kuona kama si uvumilivu wa Mungu kwetu hakuna ambaye angeokoka bali tungeangamia. Kwa hiyo yatupasa kuujali wokovu ambao Mungu aliuleta kwa kumtuma Yesu Kristo ili tupone tusije tukahukumiwa, andiko linasema, “Sisi je tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitishwa kwetu na wale waliosikia.” Ebr 2:3.

Uvumilivu wa Yesu.
Yesu kristo aliona katika kanisa la Thiatra mwanamke aitwaye Yezebeli ambaye aliyejiita nabii. Alikuwa anafundisha mafundisho ya uongo na baadhi yao waliyakubali na kuyafuata, ndipo Yesu akawapa muda wa kutubu kabla ya kuleta hukumu  juu yao. “Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke, yeye ajiitaye nabii na kuwa fundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. Tazama nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote wajue ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na moyo.Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadri ya matendo yake.” Ufu 2:20-23.Tumeweza kuona katika maandiko hayo ambayo ni kwa mfano wa kanisa la sasa, ambapo Bwana wetu Yesu Kristo analiangalia kanisa,  anawahesabia haki na wale wasiostahili watahukumiwa.   

Jinsi ya kuwa na uvumivu.
1. Kusubiri na kumtegemea Mungu kwa maombi
Hapa duniani pana shida au dhiki zinawapata wale wenye haki. Lakini yakupasa kusubiri na kumtegemea Mungu kwa maombi huku ukijua yeye ndiye msaada wako. “Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikiliza kilio changu.” Zab 41:1.   Wamtumainio (wanaomtegemea)  Bwana ni kama mlima sayuni, Ambao hautatikisika,wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake.”  Zab 125:1, 2.

2. Kumtegemea na kumngoja Mungu katika ahadi ya neno lake. “Nimemgoja Bwana, na roho yangu imekungoja, Na neno lake nimelitumainia. Ee Israeli, umtarajie Bwana; Maana kwa Bwana kuna fadhili (msaada)....”  Zab 130:5,7. 

3. Usiwe ni mtu wa kulaumu
Hili ni jambo lingine la muhimu na kuzingatia.  “Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.” 1Kor 10:10 “Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu  mwenzake; Kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.” Kol 3:13.

Kwa kuzingatia hayo unakuwa umejijenga katika uvumilivu, hutakuwa na mahangaiko, hofu, wasiwasi, uchungu na kukata tamaa.  Ndipo litatimia kwako lile neno lililoandikwa, “Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini.” Fil 4:4

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...