Hili ni tunda la Roho ambalo ni muhimu kwa kila mkristo aliyeokoka
kuwa nalo. Hii ni furaha inayotokana na Mungu mwenyewe. “....Kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe
yangu; Nitakusifu kwa kinubi Ee Mungu wangu....” Zab 43:4.
Aina za
furaha
a. Furaha
ya hapa duniani.
Hii ni furaha ambayo mwanadamu anakuwa nayo pale anapokuwa na nyumba nzuri,
au gari, anafurahi. Anacho chakula cha kutosha na fedha, anafurahi. Hiyo ni furaha ya hapa duniani ikiwa
mtu anapata yale anayoyahitaji.
b. Furaha
inayotokana na Mungu
Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia ili
mtu aweze kuwa na furaha inayotokana na Mungu.
1. Katika Roho Mtakatifu.
Mkristo ambaye ameokoka na kujazwa
Roho Mtakatifu anakuwa na furaha katika maisha yake. Ndio maana kila aliyeokoka
akizingatia neno la Mungu linavyosema uso wake huonekana mkunjufu kutokana na
furaha aliyonayo ndani yake. “ .... Mkiisha
kulipokea neno pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu”. 1The 1:6.
2. Kulijua neno la Mungu.
Hii ni furaha ipatikanayao kwa
kujifunza, kulipenda na
kulitii neno la Mungu “Nami
nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, Ambayo nimeyapenda, ....Maagizo yako ni
furaha yangu.” Zab 119:47,
143. “Upenda haki,
umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.”Ebr 1:9.
3. Kufurahi katika dhiki.
Hapa duniani mtu anaweza kupitia
katika shida mbalimbali ambazo katika hizo hujengwa na kuimarika katika Mungu,
ikiwa anazingatia kumpenda Mungu
katika neno lake. “....Tufurahi
katika dhiki pia; tukijua yakuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi (uvumilivu);
na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti nwa moyo ni tumaini,
na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa
katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu aliyetupa sisi.” Rum 5:4.%
Maoni
Chapisha Maoni