Hili ni tunda la Roho ambalo limethibitishwa katika maandiko ya
kwamba Mungu ni wa amani na amani ya kweli inatoka kwake. “Sasa Bwana wa amani mwenyewe na awape amani
daima kwa njia zote.” 2The 3:16. “....Na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa
Yesu Kristo Bwan wetu.” 1Tim 1:2.
Kudumu
katika amani.
Ili kudumu katika amani yakupasa
kuzingatia yafuatayo:
1. Kulipenda neno la Mungu na
kulitii. “Wana amani
nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza.” Zab 119:165. “Mwanangu usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako
uzishike amri zangu. Maana zitakuongezea wingi wa siku, Na mika ya uzima na
amani.” Mit 3:1-2.
2. Kuwapenda na kuishi kwa amani na
watu na utakatifu. “Msimlipe mtu
ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini kwa
upande wenu, mkae katika amani na watu wote.” Rum 12:17-18. “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na
huo utakatifu , ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia
sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na
kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.” Ebr 12:14-15.
3. Kuwasamehe wale waliokukosea na
kuachilia makosa yao. Haupaswi kuyahifadhi na kuyakumbuka, bali uyasahau, huo
ndio msamaha ulio mkamilifu. “Mimi, naam,
mimi ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe; wala sitazikumbuka
dhambi zako” Isa 43:25. Anayesamehe anajitendea wema. “Mwenye rehema
huitendea mema nafsi yake, Aliye mkali hujisumbua mwili wake.” Mit 11:17.
Maoni
Chapisha Maoni