Neno upole linaitwa kwa lugha ya
kiyunani praytes. Kwa mkristo ambaye amemjua Mungu
inampasa kufahamu ni jambo la msingi kuwa mpole. Upole hujengwa na Mkristo
mwenyewe anapoudhiwa akivumilia na kusamehe. Katika maisha ya mkristo
aliyesimama imara katika Mungu anakutana na maudhi mengi, lakini anayashinda
kwa maombi. Hatimaye anakuwa na furaha na amani kama ilivyoandikwa; “Bali wenye
upole....watajifurahisha kwa wingi wa imani.” Zab 37:11.
Kutokana na mafundisho haya mkristo
hatafadhaishwa na maudhi bali atakuwa na utulivu ndani ya moyo wako. Hatimaye
atakuwa amesimama imara katika Kristo Yesu. Ndipo andiko lisemalo furahi na
kushangilia litatimia kwake, nalo linasema; “Heri ninyi
watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo kwa ajili
yangu. Furahini na kushangilia kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni....” Mt
5:11-12.
Ili uweze kudumu katika upole.
Yakupasa usiwe na hasira na ghadhabu
uyasikiapo maneno ya kukuumiza , usiyaweke moyoni mwako bali uyapuuze na
kuyaachilia wakati huo huo, ndipo utakuwa salama moyoni mwako, kwa sababu neno
linasema, “Jawabu la
upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.” Mit 15:1.
Unaposikia maneno yaumizayo, njia ni kuyapuuza na kuyaachilia. Hapo unakuwa umeepuka kukasirika na
kuhamaki, ndio maana imeandikwa, “Asiye
mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya kuhamaki hutukuza
upumbavu.” Mit 14:29. “Basi kila mtu na awe mwepesi
wa kusikia, bali si mwepesi wa kusem;, wala kukasirika; kwa maana hasira ya
mwanadamu haitendi haki ya M ungu.” Yak 1:19-20. “Asiye mwepesi wa hasira ni
mwema kuliko shujaa ; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu autekaye mji.” Mit 16:32.
Upole
unavyojengwe.
Upole hujengwa na kupatikana kwa njia ya kujifunza na kulishika neno la
Mungu. “Jitieni nira
yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi
mtapata raha nafsini mwenu.” Mt 11:29.
Maoni
Chapisha Maoni