Kanuni ya Mungu kuhusu kuoa na kuolewa
1. Mungu alianzisha ndoa ya watu wawili mume na mke wakati
alipowaumba. Imeandikwa, “…. Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana
na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 1:27; 2:24.
Tunaweza kuona mfano mzuri kwa
Nuhu ambaye aliku mcha Mungu yeye na watoto wake watatu wa kiume kila mmoja
alioa mke mmoja. “Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina,
yeye, Shemu na Hamu na Yafethi, wana wa Nuhu, na mkewe Nuhu, Na wake watatu wa
wanawe pamoja naye”. Mwanzo 7:13. Kwa kuwa Nuhu na familia yake
walikuwa watu wa haki, Mungu hakuwaangamiza kwa ngarika akawahifadhi salama
katika safina.
2.Aliyeamini asioane au kuolewa na asiyeamini kwa sababu
imeandikwa, “Msifungiwe nira na wasioamini, kwa jinsi
isivyo swasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya uasi na haki? Tena pana
ulinganifu gani na Kristo na Beliari? (ufisadi au uchafu) Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na
yeye asiyeamini…. Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu
alivyosema, ya kwamba, nitakaa ndani yao, na katikati yao nitatembea nami
nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu”. 2Wakorintho 6:14-16.
Lakini wale
ambao walikwisha kuoana kabla ya kuamini (kuokoka) na mmojawapo akaamini asimwache
yule ambaye hajaamini kama ilivyoandikwa “ ….iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na
mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini
na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache muwewe”. 1Wakorintho 7:12; 13
3.Mungu amezuia kuoana na jamii ya karibu kiukoo.
Imeandikwa, “Mtu ye yote wa kwenu asimkaribiye mwenziwe
aliye wa jamaa yake wa karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana”. Walawi 18;1. Ndungu msomaji maandiko yaliyosalia
sikuyaandika hapa, unaweza
kuyasoma katika biblia yako nawe utajengwa Walawi 18:2-17.
Jinsi ya kumpata mke au mume mwenye busara.
1.Hupatikana kwa Bwana. “Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia
kibali kwa Bwana. Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke
mwenye busara, mtu hupewa na Bwana”. Mithali 18:22; 19:14
2.Anayeishi sawasawa na neno la Mungu.
“Yeye aendaye kwa unyofu wake kumcha Bwana. Mithali 14:2. Hufunua kinywa chake kwa hekima, Na sheria
ya wema i katika ulimi wake”. Mithali 31:26.
3. Kumwomba Mungu kwa imani naye atakupa. “Na
huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi
yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba
tunazo zile haja tulizomwomba. 1Yohana
5:14,15. Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika
kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, na haja zenu zijulikane na
Mungu”. Wafilipi 4:6.
Hapa Neno la Mungu linatufudisha kumwomba
Mungu katika mambo yote, kwa sababu pasipo yeye hatuwezi neno lolote. Kwa
maneno mengine hatutafanikiwa katika mambo yetu bila kuomba. Ndio maana
imeandikwa, “ kila
kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa
Baba wa mianga…” Yakobo 1: 17.
Waliokwisha kuoa au kuolewa wakiwa wameamini hawaruhusiwi kuachana.
“Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza;
wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana
naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”. 1Wakorintho 7:10,11. “Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine
azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini”. Luka 16:18. Pia kila mwanamke amwachaye mumewe
akaolewa na mume mwingine azini. “Maana mimi nachukia kuachana, asema Bwana
Mungu wa Israeli…” Malaki 2:16.
Onyo kuhusu tamaa mbaya
“Mmesikia kwamba imenenwa, usizini; lakini
mimi nawaambia, kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini
naye moyoni mwake”. Mathayo 5:27;28. Andiko hili pia linawahusu wanawake. Kila
mwanamke amtazamaye mwanaume kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni. “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi
yawe safi; kwa maana waasharati na wasinzi Mungu atawahukumia adhabu”. Waebrania 13:4.
“Lakini uasharati
usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wala kutamani, kama iwastahilivyo
watakatifu Maana neno hili
mnalijua hakika, hakuna mwasharati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu
sanamu, aliye na urithi katika ufalume wa Kristo na Mungu” Waefeso 5:3;5. Maandiko haya yanaonya kila mtu asifanye uasharati.
afanyaye uasharati ni chukizo kwa Mungu, atahukumiwa na kutupwa jehanum kwenye moto usiozimika
na kuteseka milele. “Na moshi wa maumivu
yao hupanda juuhata milele na milele wala hawana raha mchana na usiku…”Ufunuo 14:11.
Maoni
Chapisha Maoni